Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya NEWSAJIRA

WAMBURA AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA POLISI

Picha
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi  Waliohamishwa ni Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Saleh Ambika ambaye amehamishwa kutoka Kitengo Maalumu cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwenda kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuchukua nafasi ya Kamishna Faustine Shilogile aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo ambaye aliteuliwa na kupandishwa cheo na Rais kuwa Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii.  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Philemon Kahabi Makungu amehamishwa kutoka Mkuu wa Operesheni mkoa wa Kigoma kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, kuchukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye 2 alipandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.  Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Janeth Magomi amehamishwa kutoka Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, kuchukua ...