KESI YA PADRI MASHAHIDI 10 KUTOA USHAHIDI
Wakati upande wa mashtaka katika kesi ya ubakaji wa mtoto wa miaka 12 inayomkabili Padri Sostenes Bahati (41) wa Kanisa Katoliji Jimbo la Moshi ukisema utaleta mashahidi 10, upande wa utetezi umeiarifu mahakama kuwa itaegemea ushahidi kuwa mshtakiwa hakuwepo eneo la tukio siku ya tukio hilo.Kisheria, ushahidi huo unaofahamika kama Alibi, ni pale mshtakiwa anapojitetea kuwa alikuwa mahali pengine wakati wa tukio hilo, na hutakiwa kutolewa taarifa mapema, ili upande wa mashtaka ujiandae kwa ushahidi huo.
Jana, Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Salome Mshasha anayesikiliza kesi hiyo ilielezwa namna kosa hilo la ubakaji lilivyotendeka Agosti 12,2022 katika Parokia Teule ya Mt Dionis Arobagita iliyopo Kawawa wilaya ya Moshi.
Comments