Posts

Showing posts from August, 2023

MKUU WA SHULE ASIMAMISHWA KWA TUHUMA ZA NGONO KWA WANAFUNZI

Image
 Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam imemsimamisha kazi Mkuu wa Shule ya Sekondari Makumbusho, Juma Mulindani kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za kuwanyanyasa wanafunzi kingono. Hatua hiyo imekuja siku nne tangu Mwananchi imeripoti tuhuma hizo zinazodaiwa kufanywa na mkuu huyo wa shule Agosti 18 mwaka huu. Taarifa iliyotolewa juzi na Manispaa ya Kinondoni ilieleza uchunguzi wa awali ulikamilika wiki iliyopita na sasa wameingia katika hatua ya pili na tatu ya kuchunguza udhibiti ubora wa elimu kabla ya kueleza kilichobainika. Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kinondoni, Mtundi Nyamhanga amesema kwa sasa wanaendelea kujiridhisha na taarifa walizozipata na watatoa taarifa rasmi mwishoni mwa wiki. “Kama mtumishi amehusika na suala hili atapelekwa Tume ya Walimu na tunapofanya uchunguzi wetu tunamuweka mkuu wa shule pembeni, anapisha kituo tufanye uchunguzi wetu na kama tukimhitaji tunamuita na kazi kubwa itafanywa na wadhibiti ubora,” amesema Ny

APANDISHWA KIZIMBANI MOSHI KWA KUIBA VIELELEZO KITUO CHA POLISI

Image
Moshi. Mbeba mizigo ‘kibega’ katika soko la Mbuyuni mjini Moshi, Jackson Mussa (20), amepandishwa kizimbani akituhumiwa kuvunja kituo cha kati cha Polisi Moshi na kuiba vielelezo mbalimbali. Katika kesi hiyo namba 151 ya 2023 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Mussa ameunganishwa na watuhumiwa wengine watano wanaotuhumiwa kukutwa na vitu vilivyoibwa katika kituo hicho cha polisi. Watuhumiwa hao ambao wako nje kwa dhamana baada ya kukana mashtaka isipokuwa Jackson Mussa ni Bakari Ibrahim (27), Charles Mmbaga (29) na Juma Mudathiri (27) wakazi wa Njoro Railway na Swalehe Abdalah (29) mfanyabiashara mkazi wa Pasua. ALSO READ Aliyeshiriki kuchanganya udongo wa Tanganyika, Zanzibar afariki Kitaifa 1 hour ago Aliyeshiriki kuchanganya udongo wa Tanganyika, Zanzibar afariki Kitaifa 1 hour ago Pia ameunganishwa Stella Oscar (24) ambaye ni Stasheni Masta wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) katika stesheni kuu ya Moshi iliyopo eneo la Njoro Railway katika Manispaa ya Moshi mkoani Ki

DC MAHAWE AWAITA WANANCHI MBOZI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU

Image
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Esther Mahawe amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ambao unatarajiwa kupokewa Septemba 4 mwaka huu katika Kijiji cha Nanyala. Mbio za Mwenge huo wa Uhuru zinatarajiwa kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo inatekelezwa na Serikali ili kuwaboreshea na kuwasogezea karibu huduma wananchi. DC Mahawe ametoa wito huo Agosti 23, 2024 akiwa katika mikutano wa hadhara kata za Nanyala na Ruanda ambapo akisema Mwenge wa Uhuru utapokewa kiwilaya katika Kijiji cha Nanyala kabla ya kuzungushwa kukagua na kuzindua miradi mbalimbali katika wilaya hiyo. “Mwenge wa Uhuru unaleta upendo, umoja na mshimkamano na unaondoa chuki baina yetu kwa hiyo tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa ajili hiyo. Kazi hii imefanywa vizuri na viongozi wetu wa zamani akina Mwalimu Nyerere na wengine wengi. Ninazidi kutoa hamasa ya ninyi wananchi kualikana kwa wingi ili kuhakikisha kwamba hiyo mikesha yetu ya Mwenge inaenda vizuri tupokee

HUYU NDIE ALIEMUUA MKUU WA MKOA WA IRINGA

Image
Ni miaka 52  imepita toka Mnyalukolo, SAID ABDALLAH SIULANGA MWAMWINDI, ammimimie risasi na kumuua aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa, marehemu Dr. WILBERT KLERUU. Mauaji hayo yaliyokea tarehe 25/12/1971 kijijini Mkungugu, Isimani, Iringa. Dr. WILBERT KLERUU alikuwa ni mzaliwa wa Mwika, Kilimanjaro ambaye alikuwa ni mmoja wa Watanzania wachache wakati huo waliokuwa na shahada ya uzamivu(PHD) ya uchumi wa kijamaa.  Dr. KLERUU alikuwa ni kipenzi cha Baba wa Taifa, Mwalimu JK NYERERE, kutokana na weledi na utendaji wake usio na mfano. Mwanazuoni mwa mwaka 1971, DR. .KLERUU alikuwaamehamishiwa mkoani Iringa kutokea Mtwara.  Dr. KLERUU alikuwa ni kiongozi machachari sana na ilikuwa kawaida kwake na alikuwa hana hiana kuwafokea hadharani watumishi wa umma wazembe. Kwa hakika,  Dr. KLERUU alikuwa mbabe sana. Akiwa Iringa, kuna wakati gari yake ilipigwa "overtake" na gari hilo lililompiga"-overtake" likamziba kwa mbele. Kufumba na kufumbua, Dr. KLERUU alishuka kama komandoo n