MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE

 


Katibu wa NEC  Itikadi  Uenezi  na Mafunzo  Taifa CCM Poul Makonda amesikitishwa na utendaji kazi wa Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe Said King'eng'ena pamoja na Katibu wa Uvccm Mkoa wa Songwe Aisha Mpuya kwa kile kinachodaiwa kuacha Majukumu yao ya msingi na kujiingiza katika vitendo vya uchochezi na migogoro baina ya Viongozi kwa Viongozi na Viongozi na Wanachama ameyasema hayo akiwa hoteli Tunduma Makonda alimuelewa wazi Katibu wa Mkoa kuacha mara moja tabia hiyo kwani taarifa zake anazo na amekuwa akihusika pia kuharibu mahusiano baina ya Viongozi wa serikali na Chama ambapo siku za hivi karibuni Katibu hiyo alidaiwa kupinga maamuzi ya wajumbe wenzie juu ya Ukaguzi wa Miradi Mkoani humo na kupindisha ratiba ya awali ya Ukaguzi Miradi hiyo


"Katibu taarifa zako ninazo unakiletea Chama taharuki unawagombanisha Viongozi wa Chama unaona haitoshi unawagombanisha pia Viongozi wa Serikali sasa nitaondoka na wewe hapa Songwe na huyu Katibu wa vu. Mkoa wote tabia zenu zinafanana na mmekuwa chanzo cha migogoro mingi hapa Songwe" alisema Makonda


Kwa upande wa Wadau wa chama wamekwenda mbali kwa Kuomba Makonda awaondoe wote wawili Mkoa Songwe na kuyaonya Makundi yaliyojitokeza Mkoani hapo ambapo mmoja kati ya Mwenyekiti wa Jumuia za Chama inadaiwa kuyaratibu na amekuwa akifanya hivyo kwa kuwachonganisha na Mwenyekiti wa CCM MKOA  Radwell Mwampashe na wamekwenda mbali kuwa zinatokea Ziara wanamkwamisha Mwenyekiti wa Mkoa kwa wao kuwa sehemu ya Watendaji wa Serikali hivyo wanaacha kazi za kukisemea Chama wanageuka wasemaji wa Watendaji walishindwa kusimamia miradi.


Mfano huyu Katibu UVCCM kila siku migogoro pale ofisini hamuheshimu Mwenyekiti wake vikao visivyomuhusu nae anakwenda bila ruhusa ni  kama ameanzisha genge lake ndani ya CCM sasa kwa Mkoa wa kimkakati kama huu aina ya Viongozi wa hivyo hawatakiwi na hili tunamuomba Makonda amchukulie hatua 


Wakati Katibu Mkoa na Katibu UVCCM wakionywa mbele ya MNEC Aden Mwakyonde  baadhi ya minong'ono iliibuka maeneo hayo ikiwataka Viongozi hao waondolewe Mkoani Songwe.

Comments

Popular posts from this blog