MFANYAKAZI NMB AFARIKI KWA KUJINYONGA

 


MFANYAKAZI wa Benki ya NMB tawi la Nkasi katika wilaya Nkasi mkoani Rukwa John Maduhu (32) mkazi wa Majengo mjini Namanyere amekutwa amekufa nyumbani kwake kwa kujinyonga kwa kamba.


Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Majengo soko kuu William Katutu alisema kuwa tukio hilo limegundulika jana asubuhi ya Mei 10,2024 majira ya saa 3 asubuhi na wafanyakazi wa benki hiyo baada ya mfanyakazi mwenzao kutoonekana ofisini asubuhi.

Alisema kuwa tukio hilo liligundulika baada ya kuchungulia dirishani katika nyumba aliyokuwa akiishi marehemu ndipo walipouona mwili ukining’inia kwenye mlango wa chumbani kwake katika nyumba aliyokuwa akiishi.

Mwenyekiti huyo wa mtaa amedai kuwa baada ya hilo walitoa taarifa Polisi ambao walivunja mlango na kuingia ndani na kumkuta marehemu akiwa amejining’iniza juu ya mlango wa chumbani kwa kutumia kamba ya jiko la umeme.

Afisa mtendaji wa mtaa huo wa Majengo Flora Mbaule amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwa katika vipimo vilivyotolewa na Daktari imeonyesha kuwa kifo hicho kimetokana na kujinyonga kwa kutumia kamba.

Mbaule amedai kuwa hadi sasa haijulikani chanzo kilichopelekea kijana huyo kujinyonga kwa maana hakuacha ujumbe wowote.

Kaimu Meneja wa NMB tawi la Nkasi Marijani James alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo ingawa hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa kuwa yeye siyo msemaji wa benki hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa Rukwa Shadrack Masija amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na ameshauri watu kuwashirikisha watu wao wa karibu pale wanapokumbana na changamoto za kimaisha badala ya kujichukulia sheria mikononi

Comments

Popular posts from this blog

ASKARI WATATU KITUO CHA TUNDUMA MAHAKAMANI KWA KWA RUSHWA