IRAN YAIONYA ISRAEL ISITHUBUTU ITAPEWA KIPIGO ZAIDI


Mkuu wa Majeshi ya Iran Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi siku ya leo Oct 02, 2024 amesema Shambulizi walilofanya dhidi ya Israel lilikuwa la kulipiza kisasi dhidi ya utawala huo ambapo asilimia 90 ya Makombora yao yalilenga

Shabaha.

“Tulivumilia uchungu wa kujizuia kwa muda mrefu lakini tuliona kwamba hawabadilishi mtazamo wao wa kujiona bora, ikiwa watafanya makosa ya kulipa kisasi kwa kuchukua hatua zozote za ziada zisizo sahihi, tutajibu mapigo kwa ukali zaidi, Katika hali hiyo, tunaweza kuamua kuharibu miundombinu yao “Bila shaka tutatetea haki zetu kwa nguvu. Wamepata jibu leo, na baada ya hili, ikiwa watafanya kosa au uovu wowote katika ngazi yoyote.”

tutajibu tena kwa ukali zaidi.”

“Katika hatua hii ya operesheni, shabaha zote zilikuwa ni za kijeshi, lakini zikienda vibaya, tunaweza kuamua kuharibu miundombinu yao vibaya pia,” alionya.

“Tunatumai kuwa utawala wa Kizayuni utapokea ujumbe

unaohitajika, na Marekani na waungaji mkono wake pia watapokea jumbe kwamba kuendelea maovu ya utawala wa

Kizayuni kutapelekea kuangamizwa kabisa, Mwenyezi Mungu

akipenda.” Alisema.

Pia aliongea kuwa Operesheni hiyo ilikuja kujibu mauaji ya

serikali ya mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh, kiongozi wa

Hezbollah Sayyed Hassan Nasrallah, na kamanda wa IRGC Abbas Nilforooshan na itaenda kuwa fundisho.

Ujumbe wa kiongozi huyo wa kijeshi wa Iran nikuwa Israel wanapaswa kukomesha uvamizi na mauaji ya watu na watoto

wasio na hatia huko Gaza na Lebanon na kuheshim mamlaka ya nchi nyingine.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE