Machapisho

MKAZI WA MOMBA ABEBESHWA KINYESI NA KUZUNGUSHWA MITAANI BAADA KUMKATA SEHEMU ZA SIRI MKEWE

Picha
 Mkazi wa kata ya Ivuna Kijiji cha kalungu Wilayani Momba anaejulikana kwa jina la Leo Simchimba amebebeshwa kikapu cha  kinyesi cha ng'ombe na nguruwe kilichochanganywa na Maji na kupitishwa mitaani na kina mama huku akichapwa viboko baada ya kudaiwa kumjeruhi mkewe sehemu za siri kwa kumkata. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa imekuwa ni desturi kwa Wakazi wa Momba pindi unapokutwa na makosa kushitakiwa kwa Viongozi wa Kimila hivyo wao ndio hutoa adhabu zikiwemo faini  ama kuzungushwa mitaani kwa kubebeshwa kinyesi kilicholewesha na kupigwa viboko. "Huyu bwana alimdhalilisha kwa kumkata kiungo cha Mkewe sehemu za siri kwa Wivu wa mapenzi na kisha kumpiga pia  Wananchi waliokwenda kuamlia ugomvi aliwatishia na kuanza kuwatukana Wana mtaa hivyo tukaamua kwenda kumshitaki kwa Wazee wa Kimila na ndipo walipotoa adhabu ya kubebeshwa kinyesi na kuzungushwa Kijiji kizima na adhabu zingine kama kulipa Mbuzi,Unga na pombe pamoja na fedha"alisema mmoja wa mas...

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Picha
 

NDEGE YAANGUKA ZIWA VICTORIA

Picha
KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera,  Maketi Msangi  amefafanua tukio la kudondoka kwa ndege katika ziwa  Victoria  takribani mita 500 kutoka barabara za kuruka na kutua ndege.   Kaimu Kamanda Msangi amesema kuwa baada ya kupata taarifa Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama wakiwemo askari maji walifika eneo la tukio wakiwa na boti mbili za uokozi pamoja na magari ya kubeba majeruhi yaliyokuwa yamepaki kando ya uwanja.   Amesema kuwa baada ya kufika walikuta kuwa ni tukio la kutengenezwa lililofanyika kwa mjubu wa taratibu na sheria za anga huku akisema wao kama jeshi waliendelea na utaratibu wa uokozi na kuokoa watu 23 kwa mafanikio.   Hata Kaimu kamanda amesema zoezi hilo mamlaka a anga imelifanya ili kuona namna gani vyombo vya usalama viko tayari kukabilia na majanga kama hayo endapo yakitokea  

MADALALI SASA KULIPA ADA,KUSAJILIWA LAZIWA UWE NA TIN,NIDA

Picha
  SERIKALI imetoa muongozo wa kusimamia shughuli za udalali nchini kwa lengo la kuwawezesha madalali kufanya kazi zitakazoleta tija kwa serikali na jamii kwa ujumla.   Muongozo huo una madhumuni ya kutambua madalali, shughuli zao, mahali wanapofanyia kazi, utaratibu wa kuratibu na kudhibiti shughuli za udalali pamoja na kulinda maslahi ya wateja, wamiliki, madalali na serikali.   Walengwa wa muongozo huo ni madalali wa nyumba, majengo, viwanja na mashamba, Serikali Kuu na serikali za mitaa, sekta binafsi, wananchi na wadau wote katika shughuli za udalali wa nyumba, majengo, viwanja na mashamba.   Hayo yalibainishwa jana tarehe 15 Desemba 2021 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alipokutana na wawakilishi wa makampuni ya uuzaji na upangishaji nyumba, viwanja na mashamba pamoja na madalali mmoja mmoja.   Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, muongozo huo unamtaka kila dalali anayepangisha, kuuza kiwanja ama au kupangisha nyumba kusajiliwa na usa...

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Picha
 

MBIO ZAMUOKOA MKANDARASI KINA WANAWAKE WAMSHAMBULIA

Picha
        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda Summary Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linawashikilia wanawake wanne kwa tuhuma za kumshambulia mkandarasi anayejenga barabara ya Nkololo Bariadi wakati wa ADVERTISEMENT By Samirah Yusuph Yusuph More by this Author Bariadi.  Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linawashikilia wanawake wanne kwa tuhuma za kumshambulia mkandarasi anayejenga barabara ya Nkololo Bariadi wakati wakifanya mila ya 'Pumbulu'. Taarifa iliyotolewa leo Desemba 14, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Blasius Chatanda imesema kuwa kundi la wanawake lilimshambulia mkandarasi (hakutaja jina) kwa kumpiga na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia majeraha. Amesema kundi hilo la wanawake walikuwa katika kutimiza mila zao za Kisukuma, ambapo mwanamke amejifungua na ikatokea mtoto amefariki huwa wanaenda kufanya tambiko hivyo wakiwa njiani wakikutana na mwanaume yoyote wanaanza kumshambulia. Taarifa hiyo ya Kamanda Chatanda i...

DARAJA MUHIMU WILAYANI MOMBA LABOMOKA

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali inafunga daraja la Chuma la Kijeshi kwenye daraja la Yara ambalo lilivunjika katika msimu wa mvua 2020/2021 na kupelekea magari makubwa kushindwa kupita. Mkuu wa Mkoa amesema daraja litafungwa muda wowote baada ya taratibu za Kijeshi kukamilika.Daraja la Yara linaunganisha mawasiliano Kati ya Chitete na Kamsamba ambapo Mabasi ya abiria na Maloli ya Mizigo hutumia daraja hilo. MWISHO.

HABARI KUBWA MAGAZETI YA LEO

Picha