Machapisho

KIJANA AJINYONGA HUKU PEMBENI AKIWA AMEACHA NGUO YA NDANI YA KIKE

Picha
  Tyson Kilasi (32) mkazi wa Kijiji cha Mawindi halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe, amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwenye goli la uwanja wa mpira wa miguu wa uliopo kijijini hapo huku pembeni akiwa ameacha nguo ya ndani ya kike.   Mwenyekiti wa Kijiji cha Mawindi, Kata ya Igima bwana Elias Mwinami amethitibitisha kutokea kifo cha kijana huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Januari 18, 2022.   Mwinami amesema chanzo cha kifo cha kijana huyo bado hakijafahamika ambapo eneo ambalo mwili wa kijana huyo wameukuta ni eneo la goli la mpira wa miguu na wamekuta nguo ya ndani ya mwanamke.   “Tumemkuta asubuhi ananing’inia kwenye goli lakini chanzo bado hakijafahamika na kimsingi tunalaani kitendo hiki ifike mahali tuelimike na hivi karibuni tu pilisi walikuja kutoa elimu kwa kweli wananchi waache kujichukulia sheria mkononi,” alisema Mwinami.   Akizungumza kwa njia ya simu Diwani wa kata ya Igima bi. Paulina Samata Mwinami amesema kata ya Igima inah...

AMUUA MKE WAKE MJAMZITO KISHA AMCHOMA MOTO

Picha
 Na Raheim Secha,Ileje MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Ilanga kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe, Subira Kibona(16) amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali mgongoni kisha mwili wake kuchomwa moto na anayesadikika kuwa mume wake, Shukrani Kamwela (16) kabla ya kutupa mabaki ya mwili huo kwenye korongo.   Kamada wa Jeshi la Polisi mkoani Songwe, ASP Janeth Magomi, akizungumzia tukio hilo jana, amesema walipokea taarifa za tukio hilo juu ya mwanamke huyo ambaye alipotea nyumbani tangu Januari 13, mwaka huu.   ASP Magomi amesema baada ya kutoonekana kwa marehemu huyo wananchi walifanya juhudi za kumtafuta ndipo walipokuta mwili wake ukiwa umetupwa katika korongo lililopo katika moja ya pori mkoani humo huku ukiwa umechomwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya mgongoni na kuchomwa moto.   Hata hivyo, ASP Magomi amesema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea kuchunguza na tayari linamshikilia mtuhumiwa. Diwani w...

HATIMAYE ZAHANATI YAKAMILIKA BAADA YA MIAKA 9

Picha
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Fyengeleza iliyoanzishwa kujengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2013 Akizungumza leo wakati alipotembelea kuona mradi huo ulioanza kazi ya kutoa huduma za afya ,Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti ameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa kutoa fedha kukamilisha mradi huo. " Mkurugenzi na timu yako nawapa pongezi kwa kukamilisha mradi huu muhimu kwa ustawi wa wananchi. Sasa huduma zinapatikana hapa karibu na makazi yao" alisema Mkirikiti Katika hatua nyingine Mkirikiti aliagiza Wakala wa Maji Vijijini ( Ruwasa) kukamilisha miundombinu ya maji kwenye zahanati hiyo mapema ili kuwezesha huduma kuwa bora. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameuagiza uongozi wa kata na kijiji cha Fyengeleza kupanda miti kwenye eneo hilo ili kuhifadhi mazingira na kuanzisha mradi wa benki tofali ili kuwezesha ujenzi wa nyumba za waganga kituoni hapo. " Diwani nataka kuona ukihamasisha wananchi wapande miti k...

KIUNGO MNAIGERIA ASEPA SIMBA

Picha
K IUNGO,  Udoh Utop  jana Jumapili  aliondoka  rasmi nchini  ambapo alikuja kwa ajili ya  majaribio ndani ya Simba na kurejea kwao nchini  Nigeria. Udoh alikuja nchini  sambamba na winga mwenye  uraia wa Ivory Coast, Cheick  Mounkoro na Sharaf Shiboub waliofanya majaribio na  Simba katika michuano  ya Kombe la Mapinduzi  lakini hakuna hata mmoja  aliyefanikiwa kupata mkataba. Akizungumza na  Championi Jumatatu, Udoh  Utop alisema kuwa tayari  ameshaondoka kurejea kwao  nchini Nigeria ambapo kuna  ofa nyingine amezipata, lakini  kama kuna timu itakuwa  ipo tayari kumsajili kutoka  Tanzania yupo tayari kujiunga  nayo. “Tayari safari yangu  imeiva na leo (jana) Jumapili  nitaondoka kuelekea Nigeria  ambapo ni nyumbani, kuna ofa nimepata kutoka timu  nyingine sehemu mbalimbali  nakwenda kuziangalia baada  ya kushindwa kusajiliwa na Simba. “Kuhusu T...

MCHUJO WA USPIKA WAIVA

Picha
  Wakati leo CCM inaanza mchakato wa kuwachuja makada wake 70 wanaoomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge, mgombea mmoja wa chama cha upinzani amejitokeza kuchukua fomu. Nafasi ya  Spika wa Bunge  iko wazi baada ya kujiuzulu kwa Job Ndugai aliyekuwa Spika tangu Novemba 17, 2015. Kwa mara ya kwanza wakati  Ndugai  akigombea nafasi hiyo, Katibu wa Bunge alikuwa Dk Thomas Kashilillah ambaye kwa sasa naye ni miongoni mwa makada 70 waliorejesha fomu kati ya 71 waliokuwa wamezichukua kuomba ridhaa ya chama kugombea nafasi hiyo. Hata hivyo, hadi CCM inaanza mchakato wa kuchuja majina ya waombaji hao, ni chama kimoja cha upinzani cha ADC kimefungua pazia na mwanachama mmoja jana alijitokeza kuchukua fomu. Mwanachama huyo, Maimuna Kassim aliyewahi kugombea ubunge jimbo la Kilindi mkoani Pwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020, alichukua fomu jana katika ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, Dar es Salaam. Maimuna alikabidhiwa fomu hiyo na Kaimu naibu katibu mkuu...

RC MGUMBA:WATUMISHI WA UMMA WAPENI MAJIBU SAHIHI WATU MITANDAONI

Picha
S SONGWE: Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amewataka watumishi wa Serikali na viongozi kwa pamoja wasaidiane kupeleka taarifa sahihi kwa umma na watanzania kuhusu mambo yanayofanywa na Serikali ili kuepuka upotoshaji. Mkuu wa Mko a amesema ayo Kwenye kikao kazi cha watumishi wa Halmashauri na Wilaya pamoja na Taasisi kutoka Mkoa wa Songwe, 14 Januari 2022. "Kitendo cha kuwaachia viongozi tu ndio waweze kutoa ufafanuzi kwa mambo yote ambayo yamefanyika na Serikali tutakuwa hatujatimiza wajibu wetu vizuri kama viongozi na watumishi wa Mkoa wa Songwe" Omary Mgumba. Mkuu wa Mkoa amesema inashangazwa unakuta mtumishi wa Serikali kwenye mitandao naye anaipinga mambo ya Serikali akiamini Serikali ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Waziri au Mkuu wa Mkoa yeye anajiweka kando kwamba sio sehemu ya Serikali na badala yake anakuwa sehemu ya kuishambulia Serikali kwenye mitandao uko ni kutojutanbua kwa mtumishi wa Serikali. Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary amesema Mtumishi w...

MBEYA CITY YAINYANGURAA SIMBA

Picha
  MECHI ya Ligi kuu Tanzania Bara imemalizika katika Dimba la Sokoine jijini Mbeya huku Mnyama Simba akiambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mbeya City.   Goli la Mbeya City limefungwa na mshambuliaji Paul Nonga dakika 20 , kwa upande wa Simba walikosa mkwaju wa Penati kupitia kwa Chris Mugalu.   Nahodha wa Mbeya city Mpoki Mwakinyuki alitolewa kwa kadi nyekundu katika kipindi chanza dakika ya 43 ya mchezo na kuwafanya kucheza pungufu mpaka mwisho wa mchezo.   Kwa matokeo hayo Simba imebaki na alama 24 bada ya kucheza michezo 11 huku Yanga ikiongoza ligi hiyo  alama 32

WAZIRI TAMISEMI ARIDHISHWA NA KASI YA UANDIKISHWAJI KIDATO CHA KWANZA

Picha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ameonesha kuridhishwa na undikishwaji na kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza huku akisisitiza kuwa Serikali imeanza mchakato wa kuajiri walimu na kuongeza matundu ya vyoo katika shule za umma. Waziri Bashungwa ameyasema  hayo leo jijini Dodoma  wakati wa ziara ya kutembelea shule ya Sekondari ya Chamwino iliyoko katika Halmashauri ya  wilayani Chamwino Kwa lengo la kujionea wanafunzi walioripoti shule kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na msingi ambao wamenufaika na ujenzi wa madarasa 15,000. Amesema baada ya Serikali kukamilisha madarasa kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeanza mazungumzo na wizara ya utumishi kwa ajili ya kuajiri walimu sambamba na ujenzi wa matundu ya vyoo. Aidha, amewaagiza wakuu wa Mikoa, Wilaya, wakurugenzi wa halmashauri  na maafisa elimu wa ngazi zote kuhakikisha wanasimamia kazi nzuri iliyofanywa na Rai...

SOMA HII TAFADHALI ISIKUPITE

Picha
 Hebu tupate funzo kidogo   Jana jioni nilipata mwaliko nyumbani kwa rafiki yangu mmoja ambae pia ni kapteni wa JWTZ kikosi cha anga (Air Transport Station) hapo Majumba sita. Baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya huku Kitunda, akanijuza anahitaji nimpe namba ya shemeji yangu flani. Nikataka kujua anaitaka ya nini? Bila kusitasita, akanijuza kwamba anauza nyumba yake iliyopo maeneo ya Kivule ili wagawane malipo na mkewe!! Nikashtuka sana, zaidi ya nilivyoshanga.....! Nikamuuliza kivipi ilhali mnaishi pamoja kwa ndoa halali ya kikristo? Akanijibu "Tumetengana tangu mwezi November!!" Hili jibu likanipa kizunguzungu haswaa, yaani zaidi ya kushtuka na kushangaa awali sasa nikapata kizunguzungu. Awali nikahisi labda ananitania na kwamba tayari pombe ilikuwa inaanza kufanya brain changes zake (maana hawa wajeda wakilewa hawaishagi kufanya vituko vya kuchekesha) lakini akasisitiza kabisa kwamba hatanii wala hafanyi mzaha bali yupo seriously!! Nikataka kujua ipoje hadi kufikia hat...

RAIS AFARIKI DUNIA

Picha
  Rais wa Mali aliyeondolea madarakani Ibrahim Boubacar Keita amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Januari 17, 2022 akiwa na umri wa miaka 76, familia yake na rafiki zake wamethibitisha kifo hicho na kusema Keita amefariki majira ya saa 600 usiku kwa saa za Afrika Mashariki nyumbani kwake mjini Bamako.   Itakumbukwa kuwa, Miaka miwili iliopita, Keita aliugua kiharusi lakini chanzo cha kifo chakehakijawekwa wazi mpaka sasa.   Keita aliiongoza Mali kwa miaka saba kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2020, wakati alipopinduliwa kufuatia maandamano makubwa dhidi ya serikali kutokana na jinsi alivyolishughulikia suala la Wanajihad.   Mgogoro wa kiuchumi na uchaguzi ulio huru pia ulisababisha maandamano hayo dhidi ya utawala wake. Keita alihusika katika siasa kwa zaidi ya miongo mitatu, akihudumu kama waziri mkuu wa nchi hiyo tangu mwaka 1994 hadi mwaka 2000

MABOMU YA MACHOZI YALINDIMA DAR

Picha
  Polisi mkoani Dar es Salaam wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) ambao wameandamana na kufunga barabara iliyopo karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Amos Makalla wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua usiku wa kuamkia jana Jumapili.   Wafanyabiashara hao maarufu machinga wamefunga barabara hiyo muda mfupi baada ya kuandamana mpaka kwenye geti la kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam huku wakidai kuwa wanataka RC Makalla atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.   Kabla ya kufunga barabara, wafanyabiashara hao ambao baadhi yao walikuwa wamebeba mabango waliandamana huku wakiwa wanaimba “Tunataka Soko letu” wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo, ikiwa ni siku moja imepita tangu soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.   Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija aliwaomba wafanyabishara hao kuwa wavumilivu na kufuata utaratibu ulio...

BREAKING NEWS:MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATANGAZWA

Picha
  Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Jumamosi, Januari 15, 2022 limetangaza matokeo ya Upimaji wa Kitaifa kidato cha Nne, mitihani iliyofanyika Novemba 2021. NECTA pia imetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, mtihani wa maarifa, kidato cha pili na darasa la nne. Bonyeza kila kiungio hapa chini kuona matokeo husika; MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2021 MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2021 MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2021 MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2021

HATIMA YA SABAYA KUJULIKANA LEO

Picha
  Arusha. Hatima ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita iwapo wana kesi ya kujibu au la inatarajiwa kujulikana leo. Januari 10, Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili sabaya na wenzake alisema leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha itatoa uamuzi huo baada ya jamhuri kufunga kesi kwa upande wao. Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule aliieleza shauri lilipangwa kwa ajili ya kusikiliza ila upande wa jamhuri wanaomba kufunga kesi dhidi ya washtakiwa hao. Wakili wa utetezi, Mosses Mahuna alieleza kuwa hawana pingamizi na ombi lililowasilishwa na kuwa licha ya wao kuwa na fursa ya kufanya mawasilisho kushawishi mahakama endapo watuhumiwa wana kesi ya kujibu au la, hawatatumia fursa hiyo. “Kiutaratibu mahakama inapaswa ku determine watuhumiwa kama wana kesi ya kujibu au la, na kwa upande wetu tuna haki ya kuleta submissions ili kuieleza na kushawishi mahakama endapo wana kesi ya kujibu au la. “Upande wetu...

RAIS SAMIA AKUTANA NA SPIKA MTAAFU NDUGAI IKULU DODOMA

Picha
Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu amekutana Ikulu Chamwino na aliekuwa Spika wa Bunge la Tanzania aliejiuzuru Mhe Job Ndugai Jiji Dodoma Tanzania  

NAPE ATOA SIKU 7 WAANDISHI WA HABARI KULIPWA

Picha
  SERIKALI imetoa siku saba kwa waajiri wote wanaodaiwa na waandishi wa habari waliofariki katika ajali ya gari wilayani   Busega   kulipa stahiki zao.   Agizo hilo limetolewa na  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye  wakati wa hafla ya kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa waandishi watano na dereva wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza waliofarika dunia jana.   “Nimepewa salamu hapa kuwa miongoni mwa waliolala kwenye majeneza hapa mbele yangu hawajalipwa stahiki zao; natoa siku saba kwa waajiri wote wanaodaiwa kulipa stahiki zote za marehemu na kutoa taarifa ofisi ya mkuu wa mkoa,” ameagiza  Nape .   Akionyesha msisitizo kuhusu agizo hilo, Waziri huyo aliwataka wamiliki wa vyombo vya habari waoadaiwa kutambua kwamba wizara yake ndiyo imeshikilia leseni zao.   “Yawezekana kuna hali ngumu ya kiuchumi, lakini nasema stahiki zote za marehemu hawa zilipwe ndani ya siku saba. Hayo ya hali ngumu tutayazungumza huko m...

NAPE AWAAGIZA POLISI KUCHUNGUZA AJALI ZA WAANDISHI WA HABARI

Picha
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuchambua matukio yote ya ajali za barabarani kwenye misafara ya viongozi nchini ambayo yanachukua maisha ya wana tasnia hiyo.   Amesema hayo wakati akitoa pole kwenye hafla ya kuaga miili ya wanahabari watano mkoani Mwanza; “Nilipokuwa nakuja huku wakubwa wangu wamenielekeza kuwa nifuatilie hili la ajali kwenye misafara ya viongozi, kwanini waathirika wamekuwa ni waandishi wa habari, lazima tujue chanzo ni nini?   “Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda,” amesema. Nape amesema baada ya kukabidhiwa taarifa ya uchunguzi mambo mengine yatafuata ikiwemo kubadilisha utaratibu mzima na kwamba utaandaliwa utaratibu maalumu au itifaki rasmi ya namna bora ya ushiriki wa wanahabari kwenye ziara hizo. ...

MCHEZAJI WA TANZANIA KUTUA BARCELONA

Picha
NYOTA mwenye asili ya Tanzania, Akram Afif ametajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha wa Barcelona, Xavier Hernandez amepanga kuwasajili mwishoni mwa msimu wakati wa kiangazi kwa ajili ya kukijenga upya kikosi chake.   Xavi anaamini kuwa Afif ambaye baba yake ni Mtanzania aliyewahi kuichezea Simba, anaweza kuongeza makali kwenye kikosi chake kama ilivyokuwa Qatar.   Kocha huyo wa sasa wa Barcelona, anamfahamu vizuri Afif kwani wawili hao waliwahi kufanya kazi pamoja tena yenye mafanikio makubwa kwenye klabu ya Al Sadd.   Ripoti kutoka Qatar zinasema kuwa Barcelona wanamfuatilia kwa karibu winga huyo wa kushoto mwenye miaka 25 na wapo tayari kuweka mezani Euro 2.70m (Sh7 bilioni).   Kama Barcelona watapata saini ya winga huyo basi hii itakuwa awamu ya pili kwa Afif kucheza Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, awamu yake ya kwanza aliichezea Villarreal.   Winga huyo mwenye asili ya Tanzania amekuwa kwenye vichwa vya habari huko Qatar kwa kipindi kirefu kutokana ...