NAPE AWAAGIZA POLISI KUCHUNGUZA AJALI ZA WAANDISHI WA HABARI

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nauye ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuchambua matukio yote ya ajali za barabarani kwenye misafara ya viongozi nchini ambayo yanachukua maisha ya wana tasnia hiyo.

 

Amesema hayo wakati akitoa pole kwenye hafla ya kuaga miili ya wanahabari watano mkoani Mwanza; “Nilipokuwa nakuja huku wakubwa wangu wamenielekeza kuwa nifuatilie hili la ajali kwenye misafara ya viongozi, kwanini waathirika wamekuwa ni waandishi wa habari, lazima tujue chanzo ni nini?

 

“Tupitie ajali zote zilizohusisha wanahabari kwenye misafara, viongozi wangu wameniagiza tuwaombe wenzetu wa jeshi la polisi watuletee ripoti za ajali hizi tuone kwanini zinagusa wanahabari na tuchukue hatua ya kuwalinda,” amesema.

Nape amesema baada ya kukabidhiwa taarifa ya uchunguzi mambo mengine yatafuata ikiwemo kubadilisha utaratibu mzima na kwamba utaandaliwa utaratibu maalumu au itifaki rasmi ya namna bora ya ushiriki wa wanahabari kwenye ziara hizo.

 

Kauli hiyo ya Nape imejibu kilio cha wanahabari wengi nchini kuwa mara nyingi hawapewi kipaumbele kwenye ziara hizo, ambapo mara nyingi wanapewa magari yasiyo na viwango, ambayo hayawezi kuendana na mwendo wa misafara yenyewe na kujikuta yakiachwa nyuma na pale wanapojitahidi kukimbia ili kuwahi matukuio wanaishia kupata ajali na kupoteza maisha

 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO