Machapisho

POLISI YAONYA WANAVAA MAVAZI YA KIJESHI

Picha
  Jeshi la Polisi Tanzania limewataka Watu wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama kinyume na sheria za Nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitosita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya Watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya Walinzi wa Viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama” “ Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza Mtu yeyote ambaye sio Askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za Majeshi, sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza pia Mtu yeyote ambaye hatumikii Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala Jeshi lolote lililowekwa kwa mujibu wa sheria kuvaa vazi rasmi la Jeshi lolote katika hayo yaliyotajwa au vazi lolote linalofanana na vazi rasmi la Majeshi hayo au kuwa na alama ya kiaskari au al...

ADONDOKA KUPITIA DIRISHANI GHOROFANI AKIDHANI MLANGO MOROGORO

Picha
 Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Rogan, ameanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi ya pili katika Hoteli ya Cate iliyopo eneo la Kitungwa barabara ya Morogoro - Dar es Salaam, baada ya kupitia dirishani, huku akidhani ni mlango wa kuingia chooni. Morogoro. Katika hali ya kushangaza, mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Rogan, ameanguka kutoka ghorofa ya tatu hadi ya pili katika Hoteli ya Cate iliyopo eneo la Kitungwa barabara ya Morogoro - Dar es Salaam, baada ya kupitia dirishani, huku akidhani ni mlango wa kuingia chooni. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Mkaguzi Emmanuel Ochieng, amethibitisha kwa kusema: "Tukio hilo limetokea leo alfajili na kwamba askari wa jeshi hilo walifika na kumuokoa mtu huyo ambaye alikuwa amekwama ghorofa ya pili." Kamanda Ochieng amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wahusika wa hotel hiyo, ilibainika kuwa mtu huyo alifika hotelini hapo jana akiwa na mke wake na walichukua chumba...

RIPOTI YA HAKI JINAI YAWATAKA MARC NA MADC KUTOJITAMBULISHA KAMA WENYEVITI WA ULINZI NA USALAMA

Picha
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema kuwa wakuu wa mikoa, wilaya ni kosa kisheria kujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya Ulinzi na Usalama. Dar es Salaam. Tume ya kuboresha mfumo na taasisi za haki jinai nchini imebaini kuwa wakuu wa mikoa na wilaya hujitambulisha kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama kinyume na sheria inayowatambua kama wenyeviti wa kamati za usalama.  Pia, Tume hiyo imebaini kuwa wakuu hao huambatana na kamati za usalama katika ziara zao hali inayosababisha hofu kwa wananchi na kuwafanya washindwe kufikisha kero zao kwa kuogopa kukamatwa, kuongeza gharama kwa Serikali kutokana na matumizi ya magari na posho wanazolipwa watumishi hao kwenye ziara hizo. Akisoma taarifa rasmi ya Tume leo Jumamosi Julai 15, 2023 Ikulu Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema Tume imependekeza wakuu wa mikoa na wilaya wasijitambulishe kama wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama. Amesema ...

CHONGOLO SUALA LA BANDARI NI CCM

Picha
 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu mkataba wa uwekezaji bandarini kwa sababu utakuwa na manufaa mengi ta Taifa.  Amesema mkataba huo ni wa CCM sio mtu mmoja na amesisitiza kuwa suala hilo lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020, ibara ya 59 na ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa bandari. Chongolo amesema hayo leo Julai 15, 2026 wakati akihutibia wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Ruanda Nzovwe, jijini Mbeya. Amesema kuna watu wametengeneza uongo ili kusapoti dhamira ya kupotosha uboreshaji wa bandari nchini. “Serikali imepewa msukumo na chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, naagiza Serikali ichakate haraka kuelekea kwenye mkataba wa uwekezaji wa bandari,” amesema Chongolo na kuongeza. “Kazi ya maneno ya siasa ni ya wanasiasa, watendaji wasihangaike kujibu. Eti jambo la fulani hata angekuwa nani ndani ya CCM, agenda i...

PICHA:Uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya ccm 2020-2023 Kwenye kikao cha halmashauri kuu ya ccm wilaya

Picha
 Uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya ccm 2020-2023 Kwenye kikao cha halmashauri kuu ya ccm wilaya

LESENI YA UCHIMBAJI MADINI YA RARE EARTH ELEMENTS YATAMBULISHWA RASMI KWA WANANCHI SONGWE

Picha
Wananchi wa Wilaya ya Songwe wametambulishwa uwepo wa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya Rare Earth Elements yanayotumika katika teknolojia ya kisasa ambayo yataisaidia dunia kupunguza changamoto ya athari za hewa ya ukaa (hewa sumu) kwa kutumia teknolojia safi itokanayo na madini hayo na kuepuka athari za mazingira kwa watu na mimea. Hayo yamebainishwa na Dkt. Kiruswa katika hafla ya kutambulisha rasmi kwa wananchi Leseni ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Rare Earth Elements iliyofanyika katika Kijiji cha Ngwala wilayani Songwe.  Amesema Madini ya Rare Earth Elements ni miongoni mwa madini muhimu na ya kimkakati yanayohitajika sana duniani hususan katika matumizi ya maendeleo ya teknolojia ikiwemo utengenezaji wa betri za magari ya umeme, vifaa vya Simu, mota na teknolojia za kisasa. Aidha, Dkt. Kiruswa amesema uwekezaji katika Mradi wa Ngualla unatarajiwa kugharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 486 na utazalisha ajira rasmi 800, ajira zisizo rasmi 3,000 katika kipindi cha...

VIJANA BBT WATEMBELEA MAANDALIZI YA 88 KITAIFA MBEYA, MBOZI WAWAITA KUWEKEZA FURSA ZIPO

Picha
Na Omary Ngala, Mbeya  Vijana wa BBT MATI UYOLE wametembekelea katika Mabanda yalio katika maandalizi ya maonyesho ya 88 kwa mwaka 2023 yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mbeya. BBT  wameweza kutembelea mabanda mbalimbaki kwa lengo la kujifunza shughuli za kilimo pia kuangalia maandalizi ya siku hiyo muhimu kwa wakulima itakayofanyika kitaifa Mkoani Mbeya Vijana hao wakiwa katika moja ya banda la Halmashauri ya Mbozi ambapo Afisa Kilimo,mifugo na uvuvi (DALFO)  Wilaya ya Mbozi George akiwa ameambatana na Afisa Mwingine Anna Midigo  akiwapa maelekezo juu ya Shughuli mbali mbali za kilimo zinazofanyika Bandani hapo na jinsi walivyojiandaa na Maonyesho ya 88. Aidha Afisa Kilimo amewaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana Wilayani Mbozi za kilimo, ufugaji na uvuvi ambapo amewaeleza kwa sasa kilimo cha umwagiliaji ndio kinahitajika sana Nchini Tanzania hivyo Wilaya ya Mbozi inahitaji sana Wadau wa Vifaa vya Umwagiliaji kwa ni moja ya mahitaji kwa sasa pia amewaeleza fursa zing...

ALIEOA WAKE WATATU KATAVI MATATANI KWA KUTOKAMILISHA MIRADI YA BOOST

Picha
 Katavi. Athuman Yengayenga aliyefunga ndoa na wake watatu hivi karibuni mjini Mpanda ameingia matatani baada ya kushindwa kukamilisha kandarasi ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Mnyagala wilayani Tanganyika. Yengayenga ni kati ya watu wawili waliochukua kandarasi ya ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika shule hiyo, ambapo yeye anajenga vyumba vitatu vya madarasa. Akizungumza na mwananchi katika ziara ya Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Hassan Rugwa, wakati wa ukaguzi miradi ya BOOST wilayani Tanganyika, Yengayenga amesema alipata tenda hiyo kupitia jina la Majaliwa Lusambo. "Maandalizi ya harusi yangu yamesababisha mradi kutokamilika kwa wakati, niliweka mtu wa kusimamia lakini vifaa vilichelewa kufika site, msimamizi badala ya kutoa taarifa kwa maandishi yeye alitoa kwa mdomo,” amesema na kuongeza; "Mimi hakunishirikisha, kitu ambacho kilisababisha pia wahusika kutotilia manani, najenga vyumba vitatu na kila kimoja kinagharimu Sh2.4 ...

DKT MAGEMBE AWATAKA WATUMISHI WA AFYA KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI

Picha
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt Grace Magembe amewataka watumishi wa Afya katika Mkoa wa Songwe kufanya kazi kwa kuzingatia maadili huku akiwapongeza watumishi hao katika mkoa huo kwa kazi nzuri wanayoifanya. Dkt Magembe amesema hayo leo Jumatano Julai 12, 2023 wakati wa ziara ya kutembelea Kituo cha Afya cha Isansa, Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Songwe na Hospitali ya Wilaya ya Mbozi Vwawa. Amesema "Sisi wateja wetu ni wananchi wanakuja kupata huduma. Wahudumiwe kwa wakati wapate huduma bora, kama mpo bize wapeni taarifa wagonjwa na ndugu wanaosubiri" amesema  Pia, Dkt Magembe amesisitiza kufanyika ukaguzi wa mara kwa mara wa dawa, vifaa tiba na huduma zinazotolewa. " Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia anatoa pesa nyingi katika sekta ya afya, ukaguzi unasaidia kuwa na kumbukumbu halisi maana mali bila daftari huisha bila habari" amesisitiza Vilevile amewataka viongozi wa vituo vya afya na hospitali kufanya vikao na watumishi ili kujua  mah...

MBUNGE JULIANA SHONZA AFANYA MKUTANO WA HADHARA KATA YA IFWEKENYA WILAYA YA SONGWE KUELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM

Picha
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Daniel Shonza ameendelea na ziara katika Kata mbalimbali za Mkoa wa Songwe huku alitembelea Wajasiriamali wa vikundi mbalimbali alivyovianzisha na kuvipa mitaji ya Shilingi 300,000 kila kikundi  Mhe. Juliana Daniel Shonza amefanya mikutano ya hadhara Kata kwa Kata na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 na utendaji wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan  Mhe. Shonza amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha 2023-2024 Serikali imepanga bajeti ya ujenzi wa barabara ya Mbarizi hadi Mkwajukuni yenye Kilomita 86 ambayo itafungua kazi mbalimbali za kiuchumi kama usafirishaji kwa wananchi wa maeneo hayo   Vikundi vya wanawake wajasiriamali katika Kata ya Ifwekenya vinajishughulisha na Ufugaji wa Kuku, Biashara za Vitenge & Kilimo cha Ufuta na Karanga ambavyo vimewezeshwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe. Juliana Shonza Aidha, Wanawa...