DKT MAGEMBE AWATAKA WATUMISHI WA AFYA KUZINGATIA MAADILI NA WELEDI


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt Grace Magembe amewataka watumishi wa Afya katika Mkoa wa Songwe kufanya kazi kwa kuzingatia maadili huku akiwapongeza watumishi hao katika mkoa huo kwa kazi nzuri wanayoifanya.


Dkt Magembe amesema hayo leo Jumatano Julai 12, 2023 wakati wa ziara ya kutembelea Kituo cha Afya cha Isansa, Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Songwe na Hospitali ya Wilaya ya Mbozi Vwawa.

Amesema "Sisi wateja wetu ni wananchi wanakuja kupata huduma. Wahudumiwe kwa wakati wapate huduma bora, kama mpo bize wapeni taarifa wagonjwa na ndugu wanaosubiri" amesema 


Pia, Dkt Magembe amesisitiza kufanyika ukaguzi wa mara kwa mara wa dawa, vifaa tiba na huduma zinazotolewa.


" Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia anatoa pesa nyingi katika sekta ya afya, ukaguzi unasaidia kuwa na kumbukumbu halisi maana mali bila daftari huisha bila habari" amesisitiza



Vilevile amewataka viongozi wa vituo vya afya na hospitali kufanya vikao na watumishi ili kujua  mahitaji yao.


Pia, amewataka watumishi kuwa na lugha nzuri akisema kuwa lugha nzuri ni dawa kwa mgonjwa anapofika hospitalini.


"Lugha nzuri ni dawa hata kama hujampa dawa mgonwa ukimpa maneno mazuri anafarijika" ameeleza


Dkt Magembe ambaye aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Tamisema (Afya), Dkt Charles Mahela amewataka watumishi hao kuepuka masuala ya rushwa.


Amewapongeza Kituo cha Afya cha Isansa kwa kuwa na chumba maalumu cha watoto wachanga ambao wanazaliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa uzito.


Ametoa rai kwa wananchi wa Kata ya Isansa kuwapa ushirikiano watumishi wa kituo hicho ili waweze kudumu kwa muda mrefu na waweze kutoa huduma bora.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Tamisemi (Afya), Dkt Charles Mahela amewamepongeza watumishi wa afya katika mkoa huo kwa kazi nzuri na kusema kuwa Serikari imewekeza sana katika sekta ya afya.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

KUMBUKUMBU YA MAISHA YA MH. ESTER ALEXANDER MAHAWE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

*KUNDO AGOMA KUWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI VWAWA-MLOWO