Ahukumiwa Kifo Kwa Kupeleka ‘SQUID GAME’ SHULE
Taarifa za kusikitisha kutoka nchini Korea Kaskazini, ambapo jamaa mmoja aliyesafirisha kwa magendo filamu ya ‘Squid Game’ na kuuza kopi za filamu hiyo kwa wanafunzi nchini humo, amehukumiwa kifo.
‘Squid Game’ ni filamu ya Kikorea iliyotikisa dunia ambayo inaeleza namna watu wenye hali ngumu ya kimaisha walivyojikuta kwenye mchezo hatari wa watoto wakiwania fedha ambapo vifo vinahusika ili mshindi apatikane, Korea imegawanyika ambapo Korea Kaskazini inaongozwa na Kim Jong-un huku Korea Kusini ikiongozwa na Moon Jae-in.
Ripoti zinaeleza kuwa, hukumu hiyo ya kifo itakuwa ni ya kupigwa risasi, tayari mwanafunzi ambaye alinunua kopi ya filamu hiyo amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani, wakati huohuo wanafunzi sita waliokuwa wanaangalia filamu hiyo wamehukumiwa kifungo cha miaka mitanbo jela sambamba na kazi ngumu, huku walimu na viongozi wa shule wakifukuzwa kazi na kupewa adhabu ya kufanya kazi migodini.
Hizi hukumu ni sahihi?
Comments