SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON
Klabu ya Jogging ya Mkoa wa Songwe maarufu kama lango la SADC wamefanikiwa kurudi na medani zaidi ya kumi na tano baada ya kushiriki Tulia Marathon Mkoani Mbeya.
Klabu hiyo iliweza kushiriki mbio fupi na ndefu zilizofanyika Uwanja wa michezo wa sokoine uliopo Jijini Mbeya ambapo zaidi ya washiriki takribani 500 walishiriki, Mkoa wa Songwe ukiongozwa na Afisa Elimu Mkoa wa Songwe Michael Lighola pamoja na Viongozi mbalimbali.
Akiongea baada ya kumalizika kwa mbio hizo Lighola amesema amefurahi sana kwa Songwe kushiriki mbio hizo kwa zimewapa ujuzi na kuwakutanisha na wadau mbalimbali hivyo Mkoa Songwe unakwenda kuandaa mbio za Kimondo day kwa utaalamu zaidi na watawaalika wadau wengi zaidi.
"Kiukweli hizi mbio zimetujenga sana na niwapongeze wote walioshiriki mbio hizi toka Songwe wameonyesha umoja na kujitokeza kwa wingi" Amesema Lughola
Kwa upande wa mratibu wa Tulia Marathon upande Songwe Jogging Charles Mwamlima amesema kuwa washiriki wote wa Mkoa wa Songwe walikuwa katika hali kubwa ya kushirikia mashindano hayo na kiukweli ameushukuru Mkoa wa Songwe kupia kwa Katibu tawala Happiness Seneda kuwa wamekuwa bega kwa kuhakikisha wanashiriki
"Tumepata medani zaidi ya kumi na tano hivyo tunakwenda kuzipeleka kwa Walezi wetu Mkoa wa Songwe kuwashukuru na kuwakabidhi hiki tulichokileta" Mwamlima
Kwa upande wake katibu tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda amesema wanakwenda kuaanda utaratibu wa kuzipokea medani hizo katika utaratibu maalumu
Comments