MJUE DEREVA WA BASI LA MAJINJAH ANAETREND NJIA YA DAR-SUMBAWANGA

 




Kampuni ya Mabasi ya Majinjah Special hivi sasa ndio Kampuni pekee inayosifika kwa Usafirishaji wa abiria na Mizigo Nyanda za Juu Kusini ambapo Kampuni hii inamilikiwa na Mkurugenzi wake anaefahamika kwa jina la Alnanuswe Kabungo.

Leo niamua kukuangazia njia Dar es Salaam hadi Tunduma ambapo ndani ya basi namba T 961 DNE nakutana na Dereva kijana ambae anaoneka muda wote akiwa  bize na Majukumu yake. Boniface Charles Jimora ni Dereva aliejizolea umaarufu kutokana na basi lake kuwa ni moja ya basi pendwa na abiria wengi wamemuelezea Bonifce kwa mitazamo tofauti.


Sakina Ally ni Mkazi wa Tunduma yeye amedai kuwa amekuwa mteja Mkongwe wa Boni toka anaiendesha T 422 BUL "Ni Dereva mcheshi sana na mtu wa stori sana hapendi kuona abiria wake wamenuna na pindi anapokuwa haendeshi gari basi hupita kila siti na kutaka kujua changamoto kama zipo kwa abiria"

Nae Mzee Abiudi Mwinuka ambaje amejitambulisha kama mfanyabishara Sumbawanga amesema moja ya madereva waliotulia katika Uendeshaji Kijana Bonny humkosha sana na Kuna Mabasi hata usingizi hupati kutokana na rafu ya Magari lakini kwake Dereva Bonny humkosha.

Pius Kazonda wa Sumbawanga kwa Upande wake ameziasa Kampuni za Mabasi kuiga mfano wa Majinjah kuanzia huduma zao nje mpaka ndani ambapo alikwenda mbali kuwa Kuna Kampuni aliwahi panda akapewa Maji ya kunywa alipata ugonjwa wa kuharisha siku tatu na akasifia Kampuni ya Majinjah kwa kuwagawia abiria wao Maji safi na Salama ya Tukuyu springs Water yanayozalishwa na Kampuni ya Majinjah na vyanzo vyake vinaeleweka ni Mlima Rungwe hivyo ni Maji ya asili.


Boniface Charles ni Mwenyeji wa Nsonyanga,Mbeya

Comments

Unknown said…
Najitambua sana bony aiseee

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE