MTENDAJI WA KIJIJI ATOWEKA NA MICHANGO YA WANANCHI
Buchosa. Aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Lushamba kata ya Bulyaheke halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoa Mwanza Jonathani Nyakai ametelekeza ofisi ya Kijiji na kutoweka kusiko julikana baada ya kutuhumiwa na wananchi kutafuta kiasi cha Sh338,900 zilizo changwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha darasa shule ya Sekondari Lushamba.
Sakala hilo limeibuka Novemba 29 mwaka huu kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo kwenye Kijiji cha Lushamba alipokuwa akisikiza kero za Wananchi.
Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Lushamba ambaye anakaimu nafasi ya mtendaji wa Kijiji cha Lushamba baada ya mtendaji kutoweka na fedha za wananchi, Nyamagambo Malima wakati anawasoma taarifa ya kijiji hicho amesema changamoto ya mtendaji kutoweka na fedha za wananchi imekuwa kero kwao.
Amesema mtendaji huyo ametoweka sasa ni miezi saba hawajui alipo hivyo wananchi wanaziomba mamlaka husika kuchua hatua za kumtafuta na kurejesha fedha za wananchi.
" Wananchi wamegoma kuchangia fedha za maendeleo hivyo ujenzi wa Darasa la shule ya Sekondari Lushamba waliopewa kama kijiji limekwama kumalizoka hadi sasa" amesema Halima.
Kufuatia sakata hilo Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo amewahakikishia Wananchi wa Kijiji cha Lushamba kuwa fedha hizo zitarejeshwa na wananchi wataendelea na ujenzi wa darasa walikopangiwa
Comments