RC SONGWE ASHIRIKI MISA YA SHUKRANI YA ASKOFU MSAIDIZI ILIOFANYIKA VWAWA


Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameshiriki pamoja na waumini wa Kanisa la Roma Katoliki Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani ya Askofu Msaidizi Stephano Msomba  wa Jimbo Kuu la Dar es salaam

Misa hiyo imefanyika katika Parokia ya Mt. Patrick  Vwawa lililopo Wilaya ya Mbozi katika Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Leo Novemba 26.


Misa imeongozwa na  Mhashamu Askofu msaidizi Stephano Msomba akishirikiana na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Mbeya Na Raisi wa Baraza la Maaskofu Tanzania Gervas Nyaisonga.

Katika hotuba yake Mkuu wa Mkoa amewaomba Maaskofu Mambo mawili kwanza ni kuhusu Lambalamba ambapo amesema kumeibuka kundi kubwa la Imani za kushirikiana Mkoani Songwe na pia wapo waumini wanaoshiriki Vitendo hivyo ameomba kupitia Maaskofu kuwakumbusha Waumini uwepo wa Mungu na kuwaonya kuacha mara moja tabia ya ramli chonganishi.aidha pia amewaomba Maaskofu kusaidia kuwaeleza Waumini kuhusiana na Janga la ukataji miti Mkoani Songwe na Uchimbaji mikaa kuwa hivi sasa vitendo hivyo vimeshamili na vinahatarisha Uhai wa Misitu hali inayopelekea jangwa
Katiba Ibada hiyo pia ilihudhuliwa na Kiongozi wa Kimila Mkoa wa Songwe Chifu  Nzunda ambapo aliwapongeza kanisa la Romani kwa kutowabagua Viongozi wa Kimila na akatumia nafasi hiyo pia kumueleza Mkuu kuwa Machifu wameamua kupambana na Lambalamba Mkoani Songwe na wapo tayari kuwafukuza kabisa kwani hata kwao Machifu watu hao ni hatari mbele ya utawala wao na watazunguka Mkoa Mzima kuhakikisha wanawaondoka kwa taratibu za kimila


Askofu Msomba amezaliwa Kijiji cha Malonji kilichopo Kata ya Ihanda Wilaya ya Mbozi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE