MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14
MBUNGE wa Jimbo la Momba Mkoani Songwe Mhe. Condester Sichalwe (Mundy) ametenga kiasi cha shilingi milioni 28 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi za CCM kwenye kata zote 14 za jimbo hilo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM kata za Nkangamo na Msangano, Mbunge Sichalwe amesema lengo la kutoa fedha hizo ni kuunga mkono shughuli za maendeleo za kujenga chama hicho.
Akiwa mgeni mualikwa kwenye kikao hicho katibu wa CCM wilaya ya Momba Kataba Sukuru, amempongeza na kumshuru Mbunge Condester Schalwe kwa kutoa fedha hizo kwa madai kuwa anajenga chama kwa vitendo.
“Tukushuru sana Mheshimiwa Mbunge jambo hili unalofanya nikubwa sana, kutoa milioni mbili kila kata si jambo dogo, inaonyesha ni jinsi gani unavyokipenda chama chetu, hakika wewe ni Mbunge wa mfano sana” Kataba.
Kupitia mpango huo tayari Mbunge ametoa milioni Nne kwa kata mbili za Nkangano na Msangano, huku akiendelea na kata zingine, lengo ni kuona kata zote zinafikiwa na fedha hizo.
Comments