WALIMU NA WANAFUNZI WAPANGA FORENI CHOO KIMOJA
Sengerema. Shule za msingi nne katika Wilaya ya Sengerema zina upungufu wa vyoo hivyo kulazimika wanafunzi kutumia choo kimoja na walimu.
Shule hizo ni pamoja na Kizugwangoma, Sengerema, Nyampulukano na Mweli ni zenye upungufu wa matundu ya vyoo 60 hali inayopelekea walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.
Shule hizo zinazokadiwa kuwa na zaidi ya wanafunzi 4500 zimekumbwa na kadhia hiyo ya upungufu wa matundu ya vyoo hivyo kuleta adha ya walimu na wanafunzi kupanga foleni kwenye choo kimoja Ili kupishana kupata huduma ya kujistiri.
Diwani wa Kata ya Mishine, Mbugai Majumba ametembelea shule ya msingi Kizugwangoma leo Jumapili Novemba 28, 2021 na kubaini shule hiyo kuwa na upungufu wa matundu ya vyoo 15.
Shule ya Msingi Kizugwangoma yenye wanafunzi wanafunzi 1252 na walimu 28 ina matiundu ya vyoo 8
Kutoka na kukabilia na hali hiyo wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali ili kusadia shule hizo lengo ni kuondoa foleni za walimu na wanafunzi kutumia choo kimoja.
Comments