DIWANI MLOWO AUPIGA MWINGI AFUNGA MWAKA KWA STAILI YAKE
Diwani wa kata ya Mlowo kata iliobeba Makao makuu ya Mkoa wa Songwe Mheshimiwa Jackson Mwanda amefunga mwaka kwa staili yake baada ya kufanya Mkutano mkubwa wa hadhara Kijiji cha Ivanga na kukusanya mamia ya Wananchi.
Mkutano huo uliohudhuliwa na Viongozi wa Chama Wilaya wakiongozwa na Katibu Mwenezi Wilaya ya Mbozi Zawadi Shombe na kwa upande wa Viongozi wa Serikali akiongozwa Teo wa Mji wa Mlowo ambae pia ni Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Joel Kaminyoge.
Mhe Mwanda alianza kwa kuyaweka bayana yale Serikali ilichokifanya katika kata yake ikiwemo Ujenzi wa Madarasa,stendi ya Wilaya ambapo amesema mamilion ya pesa Serikali imetoa kwa kata Mlowo ili kukamilisha na kuanzia miradi mbalimbali.
Wakati huo huo amekemea tabia ya baadhi ya watu kubeza mafanikio yanayofanywa na Serikali ikiwemo na kumbeza yeye mwenyewe na kudai watu wa aina hiyo wapuuze na ni urafi tu wa madaraka wa baadhi ya watu ndio unaowasasumbua.
Kwa upande wa Wananchi walimpongeza Diwani wao kwa kufanya Mkutano na kuwajibu maswali yao kwa ufasaha na hawajutii kumchagua
"Huyu Diwani ni shapu sana na anajituma leo katujibu maswali yetu kwa umakini bila shaka wana Mlowo tulichagua mtu sahihi hao wa kubeza tunawajua ni ugulugulu tu unawasumba"alisema mama Shitindi wa Mlowo
Aidha kwa hatua nyingi kabla ya kufanyika mkutano huo kulifanyika michezo mbalimbali kama ya kufukuza kuku na zawadi mbalimbali zilitolewa.
Comments