KUCHOMA MATAILI MARUFUKU SONGWE
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe kuwapima kilevi madereva wote wa vyombo vya moto katika kipindi iki cha sikukuku za Christmas na mwaka mpya ili keupuka ajali.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo ilo wakati akitoa salamu za sikukuu za Christmas na mwaka mpya kwa wananchi wa Songwe akiwa Tunduma, 24 Desemba 2021.
"Madereva wasiendeshe vyombo vya moto wakiwa wamelewa na kama umekunywa ni bora upaki gari pembeni usubiri pombe iishe" Omary Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amewataka madereva wa vyombo vya moto kufuata sheria za Usalama Barabarani ili kuepuka ajali za Barabarani ambazo zinaweza kugharimu maisha ya watu.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku kuchoma mataili na kulipua milipuko ambayo inaleta taharuki kwa sababu kuna watu hawawezi kuimiri pia ametahadhali kuchukua hatua za Ugonjwa wa UVIKO-19 pindi wawapo kwenye maeneo ya kumbi za starehe na maeneo mengine ya Mkusanyiko katika kipindi hiki cha Sikukuu.
Aidha Mgumba awewatakia wakazi wa Mkoa wa Songwe sikuku njema za chrismasi na Mwaka mpya washehereke kwa amani na utulivu pia Vyombo vya Ulinzi vipo tayari kuhakikisha amani inakuwepo kipindi chote
Comments