MOMBA WAMKOSHA RC SONGWE UJENZI WA MADARASA YA COVID 19
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amefanya ziara ya siku moja Wilayani Momba.Akiwa Momba Mgumba amefanya Ukaguzi wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Shule ya Sekondari Nkangamo yenye Jumla ya Wanafunzi 337 ambapo Kati ya hao wavulana ni 151 na wasichana ni 186.Shule hiyo ilioanzishwa mwaka 2009 ina jumla ya Waalimu 19 ikiwa 12 ni wakiume na 7 wakike.
Awali Makamu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Julither Awe alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa Shule hiyo tarehe 20.10.2021 ilipokea jumla ya fedha Milioni 60 kutoka Hazina kama fedha za kupambana Uviko 19 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa ambapo wamefanikiwa kujenga Vyumba 3 na ofisi moja ya Waalimu ambavyo vyote kwa pamoja vimeshakamilika.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Momba Regina Bieda amesema Ujenzi wa Vyumba hivyo na ofisi katika Shule hiyo umekamilika kwa asilimia 100 na kuwashukuru Wananchi wa Nkangamo pamoja na Diwani wao kwa ushirikiano waliouonyesha mwanzo mpaka mwisho wa Zoezi zima la Ujenzi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba amewapongeza Halmashauri ya Momba kwa usimamizi mzuri wa fedha za Serikali na ameridhishwa na ubora wa Madarasa hayo Matatu na ofisi
"Momba niwapongeze sana kwa kujenga Madarasa ya kiwango cha hali ya juu mmejitahidi kufanya matumizi mazuri ya fedha za serikali" alisema Mgumba.
Comments