RC SONGWE AANDIKIWA BARUA YA VITISHO
Mwananchi asiyefahamika Wilayani Momba Kata ya Myunga amemuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omari Mgumba akituhumu baadhi ya Wanakijiji kujihusisha na matukio ya Uvunjanji Amani na Vitisho kwa Wananchi.
Aidha barua hiyo iliwatuhumu baadhi ya Viongozi wa jeshi la Polisi Wilayani Momba,Diwani wa kata hiyo na Mtendaji wa kata kuwa wanajihusisha na rushwa na wamekuwa wakila njama na watuhumiwa.
Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara katika kata hiyo ya Miyunga na Wananchi hao ambapo aliwaeleza kuwa amepokea barua ofisini kwake isiokuwa na jina la Mwandishi wa muhuli wa la saini ya Mwandishi.
Sehemu ya barua hiyo inawataja ndugu wawili ambao Majina yao tunayahifadhi kuwa wamekuwa tishio Kijiji hapo na wanawatishia Wananchi wa kata ya Myunga na ikaeleza kuwa Mauaji wa aliekuwa Weo Mbozi Protus Siame waliomua walijulikana lakini walipofikishwa Polisi kesi iliishia kwa Mkuu wa Kituo Tunduma na ikadai barua hiyo kuwa Diwani na WEO wa Miyunga walipewa pesa na watuhumiwa wakaachiwa.
Akijibu tuhuma hizo Mtendaji wa kata hiyo alimueleza Mkuu wa Mkoa na Wananchi katika Mkutano huo wa hadhara alisema kilichopo Katika Kata hiyo ni Ugomvi wa Mashamba uliopo baina ya familia mbili Kati Tito Siwakwi na Mzee mmoja alifahamika kwa jina la Simfukwe na kulielezea tukio lilotokea hivi karibu la Uvamizi uliofanyika Kwa Mze doe Simfukwe ambapo Mzee Simfukwe alidai mwizi huyo kabla kuuwawa aliwataja baadhi ya Wahusika lakini walipopelekwa Wahusika Polisi waliachiwa baada ya kuonekana hakuna ushahidi dhidi yao.
Wananchi wa kata hiyo ya Myunga mbele ya Mkuu wa Mkoa wameikana barua hiyo na kusema hao wanaotajwa katika barua hiyo sio sahihi na ni watu wema ni Ugomvi tu kifamila ndio umepelekea kuandikwa kwa barua hiyo na pia wamesikitishwa Diwani wao kuchafuliwa katika barua hiyo pamoja na Mtendaji wa kata hiyo.
"Kwa kuwa mmethibitisha wenyewe kuwa haya yalioandikwa katika barua hii sio sahihi na mmesema ni Ugomvi wa kugombea Mashamba na hawa waliotuhumiwa hawahusiki nawaomba sana Wananchi msitoe taarifa za Uongo na zenye chuki sababu tu ya Ugomvi wenu binafsi,msiwachafue Viongozi wenu kama mlivyomchafua Diwani na Mtendaji wenu wa Kata nawaomba sana"alisema Mkuu wa Mkoa Mgumba
Comments