SONGWE GIRLS KUANZA RASMI JANUARI



Na Baraka Mwashambwa Afisa Habari Songwe

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songwe iliyopo Kata ya Myunga Kuanza na wanafunzi wa kutwa kwanza ifikapo Januari 2022.

Afisa Elimu Mkoa wa Songwe, Mwl. Juma Kaponda  amesema kwa miundombinu iliyopo sasa wataanza na wanafunzi wa kutwa kwanza ambao ni wasichana tu ambao watatoka jirani na Myunga wakati wakisubiria kupata fedha za ujenzi wa Mabweni na Nyumba za walimu ambazo atakaa mlezi na Mkuu wa Shule.

Afisa Elimu amesema hadi kukamilika kwa Shule itakuwa ni kidato cha kwanza hadi sita.

Mwezi Oktoba 2021 katika kikao cha maendeleo ya Elimu Mkoa kilichongozwa na Katibu Tawala Mkoa, Ndg. Missaile Musa kikao kiliazimia Halmashauri zote za Songwe kuchangia fedha kila moja Milioni 30 ili kufanikisha Shule ianze kuchukua wanafunzi ifikapo Januari 2022.


Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba amemuagiza Afisa Elimu Mkoa kukamilisha miundombinu mhimu ambayo itawezesha wanafunzi kuanza kusoma ifikapo Januari 2022.


"Lengo la Serikali ni ifikapo Januari 2022 Shule ianze na Kwa kuwa kuna fedha ambazo wadau wametoa ni vyema kamilisheni miundombinu mhimu haraka" Omary Mgumba.


Mkuu wa Mkoa amesema Shule itaanza Januari wakati Serikali ya Mkoa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa Mkoa na Serikali kuu wanafanya Jitihada za kukamilisha ujenzi wa Mabweni na miundombinu mingine iliyobaki ili lengo la Shule ya kuwa bweni kwa wasichana likamilike.


"Hadi sasa Shule hii imegharimu fedha zaidi Milioni 320 kutoka kwa wadau wa maendeleo wa Mkoa na Serikali kuu" Omary Mgumba.


Shule ya hii imeanza kujengwa 2020 kutokana na Agizo la Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluh Hassan alilotoa 2018 alipofanya ziara Mkoa wa Songwe akiwa Makamu wa Rais na kutaka Mkoa wa Songwe ujenge Shule ya bweni ya wasichana sehemu ambapo kuna mdondoko mkubwa wa wananfunzi wa kike na Mkoa ukaamua kujenga Kata ya Myunga Wilaya ya Momba.


MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE