WACHIMBA VISIMA WAANZISHA HOTEL SONGWE RC AIFUNGUA

 


Mkuu wa Mkoa amezindua hotel ya Forest Hill hotel iliopo kata ya Mlowo Wilayani Mbozi inayomilikiwa na Vijana wawili David Tuya na Christopher Mponzi wanaojihusha na Uchimbaji wa Visima maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Songwe na nchi mzim ya Tanzania.

Kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa Omary Mgumba alifanya Ukaguzi wa Ujenzi wa  Wawekezaji hao na kutembezwa maeneo mbalimbali ya hotel hiyo na kisha kusomewa risala aliyoandaliwa na mmoja wa Viongozi wa Hotel hiyo Frank Ngowi ambapo katika risala hiyo walimueleza Mgumba nia na madhumuni ya kujenga hoteli hiyo ikiwemo utoaji wa ajira ambapo mpaka sasa wameweza kuajiri wafanyakazi zaidi ya 20 na hivyo kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasani ya kazi iendelee.

Aidha katika risala hiyo pia walimueleza changamoto mbalimbali ikiwemo Umeme Mdogo unaosababisha Miundo mbinu yao ya Umeme kushindwa kufanya kazi kwa uhakika.Pia waliomuomba Mkuu wa Mkoa kuwasaidia Ujenzi wa Miundo mbinu ya Barabara kufika eneo lao ilipo hotel hiyo kuwa ni mibovu.

Mmoja Kati ya Wakurugenzi wa Hoteli hiyo Davidi Tuya ametoa kisa kimoja mbele ya Mkuu wa Mkoa kwa kuelezea historia fupi ya urafiki wao yeye na mmiliki mwenzie Christopher Tuya kuwa walianza kuwa madalali wa matofaili wakiwa Mlowo na waliendelea kuaminiana kipindi chote hicho hadi walipoanza kuchimba Visima kwa kutumia Mitambo na kwa sasa wamefahamika karibu nchi nzima ya Tanzania na mwenzie ndie alimpa wazo la kuanza Ujenzi wa Hoteli hiyo mwaka 2020


Kwa upande wake Jeshi la polisi likiwakilishwa na ASP Ester amewapongeza Vijana hao kwa kushauriana vitu vya Msingi na kuwataka  Vijana wengine waige historia ya Vijana hao na kuwasihi Vijana kuacha kushauriana mambo ya Msingi yasiokuwa na maana kama vile kula bata na Mambo yasiofaa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa aliwapongeza wawekezaji hao kwa kuja kuwekeza Songwe Wilaya ya Mbozi na pia amesema Wawekezaji hao wametoa darasa kubwa sana moja ikiwa ni kutokuchagua kazi,kutokuchagua kazi na kutokusubiri kuajiriwa na wao waliamua kujiajiri wenyewe na akawataka watu wasiidharau kazi ya Udadali na Wawekezaji hao wae ni chachu kwa Vijana wengine kuheshimu kazi ya udalali na Serikali inawandalia mfumo mzuri wa kuwatambua madalali na kuwataka madalali kuunda ushirika wao kwa vikundi ili iwe rahisi wao kutambulika na itafikia mahali wataanza kupata hata mikopo.




Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE