DC MBOZI " MBOZI JENGENI KUMBI YA KISASA YA VIKAO VYENU MADIWANI
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Cosmas Nshenye amewata Madiwani Wilayani Mbozi kwenda kujifunza na kuangalia Kumbi za Halmashauri zingine za Mikutano ili nao waweze kujenga.
Akiongea katika Kikao cha Baraza la Madiwani Mbozi Nshenye amesema ni aibu kwa Halmashauri kubwa kama Mbozi kuwa na Ukumbi wa Mikutano kama uliopo sasa ambapo amesema staili ya Kuazimana visema( Mic) ilishapitwa na Wakati hivyo Madiwani wajipange na Ujenzi wa Kumbi mpya na kisasa.
Aidha katika hatua nyingine Cosmas Nshenye amelishauri Baraza la Madiwani kufanya utafitii mkubwa sana kutafuta vyanzo vya mapato baada ya kugundua vipo ambavyo havikusanywi.
Amesema hayo Januari 25 ,2022 kwenye kikao Cha bajeti ya mwaka 2022 /2023 ambapo Ofisa Mipango wa was Halmashauri Erasto Mwasanga halmashauri itatumia zaidi ya Sh 57 bilioni katika kipindi hicho.
Mkuu wa wilaya pia amewashauri madiwani wake akilini suala la kujenga Ofisi na ukumbi mkubwa katika Halmashauri ya Mbozi
Amewataka kuwa makini kwenye vyanzo vya mapato na pia ni vyema wangefanya tafiti kubwa kwa vyanzo hivyo
Ametoa mfano was chanzo cha mapato cha machinjio akisena wanatakiwa wajue ni Mbuzi, ng'ombe, na Nguruwe wangapi wanachinjwa kwa Wilaya nzima.
Ametaka kuangalia ni mabasi mangapi yanatoka na kuingia kwani ni zaidi ya Haice tatu zinapita kwa dakika moja, lakini kwenye daftari takwimu zinakuwa tofauti na idadi ya magari yaliopita .
"Si kweli kuwa wananchi hawalipi mapato Ila zinaingia kwenye mfuko mwingine"
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya, Simon Mboya amewashauri madiwani kufanya utafitii wa kukusanya mapato katika viwanda vya saruji na kiwanda cha Marmo ambapo ameeleza kuwa Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na Madini ya Malumalu kwa kipindi cha Miaka 3 ni shilingi Milioni 3 tu ndizo zimekusanya na Halmashauri ya Mbozi ambapo amedai kiasi hicho ni Kidogo.
Akizungumza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi ,Geogre Musyani amewaomba madiwani wenzake na wenyeviti wa kamati kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ambao mpaka Sasa ni asilimia 74.
Comments