HALMSHAURI YA MBOZI
Mwekezaji wa Kiwanda cha Maparachichi Wilayani Mbozi Mkoani Songwe Bwana Tinson Nzunda ameendelea kulalamika kwa kutolipwa fedha zake za Miche ya Maparachi zaidi ya Milioni 27 anazoidai Halmashauri ya Mbozi toka 2017 licha ya agizo la Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba kuipa siku 90 Halmashauri hiyo kumlipa.
"Mkuu wa Mkoa alishawapa agizo na Vikao vyote zimeagiza nilipwe na hata Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi Mhe George Musyani alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kupitishwa malipo yangu ndani ya Vikao vyote sasa sijui Mpaka sasa kwanini silipwi?" Amesema Mwekezaji huyo Nzunda.
Aidha Mwekezaji huyo ametoa nyaraka zake zote zenye kuonyesha makabidhiano ya Miche hiyo ya Mapachichi kwa Shule za Wilayani Mbozi ambapo nyaraka hizo zikiwa na sahihi za Wakuu wa Shule na afisa kilimo pamoja na namba za simu za wapokeaji amesema Halmashauri ya Mbozi ilimuomba kama huduma ya Miche hiyo ya Miparachichi hivyo nae alitoa kama huduma kwa bei ya chini kabisa ili kuziwesha Shule nyingi kupanda Miparachichi sasa huduma yake imegeuka mateso kwake na amekwenda mbali zaidi kwa kusema Kama wanaona kumlipa fedha za maparachichi ni ngumu basi wamrudishie Miche yake ili kuepuka usumbufu wa yeye kuidai Halmashauri hiyo.
Mmoja kati ya Madiwani wa Wilaya Mbozi ambae aliomba jina lake lihifadhiwe amesema kuwa jambo hilo limeanza kupelekwa kisiasa na nyuma yake kuna wanasiasa ambao wanashinikiza malipo hayo yasifanyike kwa kumuhofia Mwekezaji huyo kuwa anampango wa kugombea moja ya nafasi za kisiasa Wilayani Mbozi jambo ambalo tulipomuuliza Mwekezaji Tinson alilikana jambo hilo na kushangazwa na akasema kuwa anashangazwa na maneno hayo na amekwenda mbali kuwa hata yeye ameyasikia maneno hayo na Cha ajabu mpaka aliwahi kuwasaidia kiuchumi nao wamejiingiza katika maneno ya kumsingia ambayo ameyaita ya kipuuzi.
"Ndugu Mwandishi juzi juzi tu hapa nimenunua mahali Mbolea na alieniuzia akaipeleka mpaka shambani kwangu lakini huyo huyo akadai mimi nilikwenda kuwahonga baadhi ya watu ili waje wanisaidie kugombea cheo hicho cha kisiasa huu si upuuzi huu" alisema Tinson
Ikumbukwe Mwaka jana 2021 Mkuu wa Mkoa wa Songwe alifanya ziara katika kiwanda cha Maparachichi cha Lima na akatoa maagizo ya Siku 90 kwa Halmashauri ya Mbozi kumlipa Mwekezaji huyo ambapo siku 90 ziliisha tarehe 15/01/2022 na Mwekezaji huyo hajalipwa mpaka sasa
Comments