MBOZI WAVUNJA HISTORIA WAKABIDHI MIKOPO KWA VIJANA BODA BODA ZA KUMWAGA


 Halmashauri ya Mbozi ilioyopo Mkoani Songwe imekabidhi Pikipiki 25  na Bajaji 25 kwa Vikundi 5 vya Vijana Wilayani Mbozi  kutoka kata za Mbalimbali  ambapo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba alikuwa Mgeni Rasmi.

Katika hafla hiyo iliofanyika Viwanja vya Halmashauri ya Mbozi ilihudhuliwa na Madiwani wa kata zote wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbozi George Musyani na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi pamoja, Wataalamu,Viongozi wa vyama vya kisiasa pamoja na Wananchi.

Mkuu wa Mkoa Mgumba aliwataka Vijana kujenga uaminifu katika Mikopo walipewa kwa kurejesha kiasi cha Mkopo walichopewa bila riba ili waweze kuaminika na kukopeshwa tena

"Niwasihi sana Vijana Serikali chini ya Rais Samia inawapenda sana na imeamua kuwakopesha Mikopo hii isiyo na riba nayi muweze kujikwamua kiuchumi na kuwaajili wengine lakini niwaombe sana mrejeshe Mikopo hii ili iwasaidie wengine na nyie muweze kukopa tena" alisema Mgumba

Aidha Mgumba amewapongeza Halmashauri ya Mbozi kwa kutoa Mkopo Mkubwa kwa Vijana amelipongeza Baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Mbozi Abdalah Nandonde.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE