NAIBU WAZIRI WA AFYA ASHTUKIZA BARAZA LA MADIWANI MBOZI


 Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel jana tarehe 28.01.2022 alifanya Ziara katika Mkoa wa Songwe na kuongea na Watumishi afya Mkoani Songwe.


Mara baada ya kumaliza ziara yake Naibu Waziri Dr Mollel aliwashtukiza Baraza la Madiwani Mbozi pale alipoingia na kuhudhulia.Akiwa ndani ya Baraza la Madiwani Dr Mollel alipata wasaha wa kuongea na Madiwani,Wataalamu na Wananchi walikuwepo ndani ya Baraza hilo.

Akitoa hotuba yake Naibu Waziri alisikitishwa na hamasa ya chanjo kwa Mkoa wa Songwe ambapo amesema Mkoa wa Songwe umeshika nafasi ya pili toka mwisho na Mkoa wa Manyala ni wa Mwisho kwa kutoa huduma ya Chanjo


"Watumishi wa Afya acheni ujuaji mwingi kaeni na wenzenu wawape mbinu za hamasa za Chanjo kaeni na Viongozi wa Vijiji.Madiwani na Watendaji Kata hamuwezi kujua kila kitu" alisema Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Mollel


Aidha kulingana na takwimu pia zilizotolewa Wilaya ya Ileje imeshika Mkia Kimkoa ambapo wadau mbalimbali wameeleza kudorora kwa hamasa kunatokana na baadhi ya Watumishi wa Idara ya afya kuweka Mazoea na Ujuaji mwingi na Wadau wamekwenda mbali zaidi kuwa mwanzo walishirikishwa lakini  zilipotoka tu pesa za hamasa ya Uviko walitengwa na Watumishi hao wa Afya wakaanza kujifanyia mambo pasipo kushirikisha Jamii husika.



WITO WETU KAMA CHOMBO CHA HABARI MKOA WA SONGWE UJITATHIMINI KATIKA HAMASA YA MAMBO MAZITO KAMA HAYA NA KUANGALIA WATU SAHIHI WA KUPEWA MAJUKUMU MAZITO KAMA HAYA TULISHAWAHI SHAURI JINSI YA KUENDESHA ZOEZI ZIMA NASI TUNAUNGANA NA WADAU ZILIPOTOLEWA FEDHA ZA HAMASA TULITENGWA NA USHAURI WETU UKAPUUZWA

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE