BAJETI YA TARURA YAKALIWA KOONI NA MADIWANI MBOZI
Madiwani wa Baraza la Mbozi wameitaka Bajeti ya Wakala wa Barabara TARURA kuzingatia Majimbo ya Mbozi na Vwawa.Katika baraza maalumu la Madiwani na TARURA kilichofanyika leo Jumanne ya tarehe 01,02,2021 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mbozi.Madiwani hayo wameshangazwa baada ya kusomewa Taarifa ya Bajeti hiyo na Meneja wa Tarura Wilaya ya Mbozi ambapo Jimbo la Mbozi limetengewa kiasi Cha shilingi bilioni 1 na Jimbo la Vwawa lenye kata nyingi limetengewa tu kiasi cha shilingi milioni 500.
DIWANI wa kata ya Nyimbili Tinson Nzunda ameomba fedha za utengenezaji wa barabara Mjini na vijijini TARULA Sh bilioni 1.5 za Jimbo la Vwawa na Jimbo la Mbozi zichanganywe na zigawiwe kwa usawa katika kata zote
Yamesemwa hayo Februari1 kwenye Baraza la usomaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022ya Utengenezaji wa barabara za vijijini na mjini
Akichangia hoja hiyo diwani wa kata ya Harungu Maarifa Mwashitete kwa kusema nikweli kabsa sio sahihi kwa Jimbo lingine lipewe Sh Bilioni 1 na lingine lipewe Sh milioni 500 anaomba fedha hizo ziletwe zichanganywe na zigawiwe kwa usawa .
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mbozi George Musyani akisisitiza kuwa majimbo yote yanaunda Halmashauri ya Mhozi na fedha zimetolewa kwa wanambozi hivyo anaomba fedha ziletwe mezani na zigawiwe kwa kata zote 29 .
Nae meneja wa TARULA Felix Ngomano amesema kwa Sasa bajeti imekuja atalifanyia kazi ikiwemo kuwajulisha Wakubwa wake
Comments