HII NDIO CHANGAMOTO ILIOIKUMBA STENDI MPYA MLOWO
Stendi Mpya ya Forest iliopo Mji mdogo wa Mlowo ambayo hivi sasa imekumbwa na Miundo mbinu ya kutoingilika ndani kwa ulahisi hali iliopelekea Magari ya Abiria na Shughuli zingine za kibiashara kufanyika kando kando ya Barabara kuu ya Tanzam.
Baadhi ya Madereva wa Mabasi na wafanyabiashara ndani ya Stendi hiyo inayoendelea na Ujenzi Mkubwa wa Vibanda vya biashara na Miundo mbinu mingine ndani ya Stendi hiyo na nje wametoa wameelezea kero wapatayo wao kutokana na Shughuli nyingi kufanyika eneo hilo walilodai ni finyu na ni hatari zaidi kutokana na kuwa pembezoni mwa Barabara hiyo kubwa ya Tanzam.
"Eneo hili ni dogo sana Magari ni mengi kwanini Halmashauri ya Mbozi wasifukie yale mashimo mbona ni kiasi tu kusawazisha kifusi Shughuli ziendelee" alisema Sambo Kitwana Dereva Daladala
Nae Mfanyabiashara wa pembezoni mwa maduka yaliopo jirani na Stendi hiyo Maria Mwasupila amesema wao kama Wafanyabiashara wa Maduka hivi sasa hawauzi kabisa kwani shughuli zote huishia huko huko pembezoni na Barabara hivyo amewaomba Viongozi wa Mbozi kuiwasaidia kurekebisha marekebisho hayo Madogo ili shughuli ziendelee kama mwanzo kuliko hivi sasa halmashauri ya Mbozi inakosa mapato
Baada ya kuwasikiliza na kupata Maoni mbalimbali tulimtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi Abdallah Nandonde ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo kwa kipindi hiki
"Ni kweli changamoto ile tumeiona na fedha za matengenezo zipo tayari ila tumepata changamoto kidogo ya Mitambo ya kurekebisha Barabara tumewashirikisha wenzetu Tarura na wadau wengine watusaidie tupate Mitambo hiyo kwa sasa Mkoa wa Songwe hauna Mitambo karibu yote tumeambiwa imechukuliwa na endapo tutapata hata kesho tunarekebisha tuvumiliane kidogo" amesema Mkurugenzi Nandonde
Comments