MWEKEZAJI MAJINJAH AZIDI KUVUTIWA NA ARDHI YA MBOZI


 Mwekezaji kutoka Igamba  Wilayani Mbozi Mkoani Songwe Alnanuswe Kabungo ambae pia ni mmiliki wa Kampuni ya Usafirishaji ya Majinjah logistics Company amemtembelea Diwani wa Kata ya Nyimbili  ambaye pia ni mwekezaji na mzalishaji wa Miche bora ya Kahawa,Miparachichi na mikademia pamoja na Mazao mengine kutoka Kampuni ya Lima.


Akiwa Kijiji cha Masangula Kabungo alifika Nyumbani kwa Mwekezaji huyo na kumpa pole yeye na Familia yake kufuatia kifo cha Mama Mzazi wa Mwekezaji huyu kilichotokea wiki iliopita Masangula.

Aidha baada Tinson Nzunda alipata wasaha wa kumuonyesha baadhi ya Mashamba mchanganyiko kwa maana ya Kahawa,Miparachi,Miakademia na Migomba kupandwa pamoja hali iliopelekea kumvutia Mwekezaji Majinjah na timu aliongozana nayo ukiongozwa na Meneja Uzalishaji wa Majinjah Logistics Kampani James Mgeni.

Sambamba na Shamba hilo Mwekezaji Majinjah alitembelea Shamba la kuzalisha Miche ya Kahawa,Parachichi na Mikademia  na kuona Jinsi Uzalishaji wa Miche hiyo pandikizi unavyofanyika na ambapo aliipongeza Kampuni ya Lima na kuahidi kuingia katika kilimo kikubwa cha Miparachichi na Mikademia Wilayani Mbozi na atafanya Shamba Mchanganyiko na kuahidi kutumia mbegu toka Kampuni hiyo ya Lima




Katika hatua nyingine Mwekezaji Kabungo ameonyesha kuvutiwa na utunzani wa Mazingira katika Kijiji cha Masangula na kuvutiwa na ardhi iliopo Kijiji hapo ambapo amemuagiza Meneja Uzalishaji James Mgeni kutafuta Mashamba maeneo hayo kwa lengo la kuyanunua na kuanza kilimo maeneo hao.

Katika hatua nyingine pia Mwekezaji Majinjah aliweza kumtembea mmiliki wa Night Club ya New bell iliyopo Mpemba Ndugu Yusuph ambae ni muuzaji wa Maji ya Tukuyu springs water katika Club yake hiyo na kuahidi ambapo ameahidi kumpa Uwakala wa Maji ya Tukuyu springs water kwa Mpemba na Wilaya Ileje sambamba na hili amempongeza kwa Kijana mdogo Yusuph kumiliki Club hiyo inayosifika kwa sasa Mkoani Songwe na ni Club pendwa na yeye Majinjah amekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha Vijana wanatimiza ndoto zao.

Pia alipata wasaha wa kutembeza Ujenzi wa Club hiyo ambao bado unaendelea.

Pia Majinjah alitembelea kata za Mlangali na Iyula  ambapo aliweza kutazama aina mazao na uoto wa asili wa maeneo hao kwa lengo la kufanya kilimo cha kisasa ndani ya Kampuni ya Majinjah

Comments

Itaongeza ajira kwa vijana na kuongeza kipato kwa wana-Mbozi sanjari na kuboreshwa kwa miundombinu na kukua kwa sekta zingine!

Kila la kheri Majinjah!🙋

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE