RAIS SAMIA AREJESHA TABASAMU KWA WANAFUNZI WA KIKE WALIOKATA TAMAA


 Kufuatia agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuli ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani la Wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo ya Sekondari kwa sababu mbalimbali zikiwemo Ujauzito na zingine nyingi kurejea Mashuleni.

Mkoani Songwe hususani Wilaya mama ya Mkoa wa Songwe ambayo ndio Makao Makuu ya Mkoa yalipo ya Mbozi Shule ya  Sekondari ya Vwawa ndio kituo maalumu cha Wanafunzi hao walioshindwa kuendelea na masomo kilipo.

Habari Jamii tumeweza kufika Shuleni hapo na kuwakuta wakiendelea na Masomo yao ambapo jumla ya Wanafunzi 22 wanaendelea na Masomo na Wameonyesha wazi kufurahia nafasi hiyo wao waliita ni adimu na  kihistoria kwao na hawakutarajia kama wangeipata ingali walikwisha kukata tamaa.

Wanafunzi hao huku wakiwa na nyuso zilizokuwa zimekata tamaa wameeleza kiunaga ubaga sababu zilizowafanya washindwe kuendelea na Masomo zikiwemo kupata Ujauzito,kulazimishwa kuolewa wengine ni Wazazi wao kushindwa kuwalipia ada kutokana na kutoweza kujimudu kimaisha na hata wengine walikwenda mbali kwa kusema wazi Wazazi wao hawakuwa na utayali wa kuwasomesha watoto wa kike.


Katika hatua nyingine Wanafunzi hao wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba kuwatembelea Shuleni hapo ili waweze kumpa Salamu Maalumu za shukrani kwa Rais Samia Hassani kwa kuweza kuwakomboa wao kutokana na kukata kwao tamaa na kuhisi kupoteza ndoto zao

Kutokana na tulichokishuhudia kwa Wanafunzi hawa tunatoa wito kwa Wazazi wote popote walipo na wana watoto wao walioshindwa kuendelea na masomo yao kuwapeleka haraka sana Vwawa Sekondari ili waweze kuungana na Wenzao katika kujikomboa kielimu kwa Elimu hii maalumu.


Mahojiano yetu na Wanafunzi hao na Waalimu wao tutayaleta kupitia chaneli yetu ya YouTube ya Habari Jamii tv hakikisha unaitafuta YouTube na unabonyeza neno Subscribe

Comments

Lucas Chambalo said…
Mama anasomesha wazazi, Mwenzake alisema hawezi kusomesha wazazi.

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE