TAKUKURU SONGWE YABAINI KUWEPO KWA RUSHWA YA NGONO SEKTA YA ELIMU SONGWE
Akiongea na Vyombo vya habari ofisi za TAKUKURU Mkoani Songwe Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe Edings Mwakambonja amesema kuwa Takukuru wamefanya Uchambuzi wa mifumo Mitatu ambayo ni Uchambuzi katika Sekta ya Elimu ambapo wamebaini kuwepo kwa mianya mingi ya Rushwa ya Ngono sekta ya Elimu.
Kamanda amesema kumekuwepo na viashiria vya Rushwa ya Ngono katika upangaji wa Vituo vya kazi,uhamisho wa ndani pamoja na utoaji wa fursa za mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu pamoja na Uteuzi wa kufanya kazi maalumu kama vile kusimamia mitihani.
"Pindi zinapotoka nafasi hizi kuna viashiria vya Rushwa ya Ngono kwa walio na mamlaka ya shughuli hizi hivyo ofisi yetu inatoa onyo na tunatarajia kufanya warsha na wadau wanaohusika na Uchambuzi huu ili kujadili namna ya kuziba mianya hii" amesema Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Songwe.
Katika hatua nyingine Takukuru Songwe wamebaini kuwa taasisi nyingi za Serikali hazifanyi manunuzi kupitia Wakala wa Manunuzi ya Taasisi za Umma (GPSA) na wao Wana mpango wa kuandaa warsha ili kuweza kudhibiti na kuziba mianya hiyo
Comments