WANANCHI WA ISELA,MLANGALI WAREJEA KATIKA MAJUKUMU YAO
Wananchi wa kitongozi cha isela kilichopo kata ya Mlangali Wilayani Mbozi Mkoani Songwe wamerejea katika shughuli zao za kila siku baada ya kukimbia Kitongijini kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi.
Wananchi hao ambao siku ya Ijumaa kundi la Wananchi lilivamia baadhi ya nyumba na kufanya uharibifu kwa kukata mazao,kubomoa nyumba na uharibifu mwingine ni baada ya Kaya zilizolengwa kudaiwa kukubali kusaminisha ardhi yao ili kulipwa fidia kupisha hifadhi Mpya ya Ngorongoro inayotarajiwa kuanzishwa maeneo hayo yalio jirani na Kimondo.
Kundi ambalo haliko tayari kuondoka na kupisha hifadhi hiyo ndilo linalodaiwa kufanya uharibifu.Mara baada ya Polisi kufika katika Kitongoji hicho Wananchi walikimbilia milimani ili kukwepa kukamatwa na kuziacha Kaya zao hali iliopelekea kitongozi kukosa watu na Shughuli mbalimbali kusimama.
Leo Jumapili Wananchi wa Kitongoji cha Isela wamerejea baada ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe David Mboya ambae alihakikishia Usalama wao na kuwataka kuendelea na Shughuli zao kama kawaida
Akiwa katika Kikao na Wananchi hao kilichofanyika leo Jumapili katika Shule ya Msingi Kimondo Mhe Mboya aliwaaeleza Wananchi hao kuwa Jeshi la Polisi kazi zake ni kulinda raia na mali zao hivyo baada ya kuridhika na kuhakikishiwa Usalama ndani ya Kitongoji hicho na wao Polisi wameondoka wanaendelea na Majukumu mengine hivyo kwa sasa ameyachukua yote waliojadiliana na atayafikisha ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ikiwezekana atamuomba kufika katika kitongozi hicho.
Mara baada ya Kikao chao na Diwani Wananchi wa Kitongoji hicho wameonekana wakirejea Majumbani mwao na wengine kuingia katika shughuli zao za kibiashara na kilimo
Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ACP Jannet Magomi amesema hali ya Usalama imeimarika na kwa sasa jeshi la Polisi linamsaka Mwenyekiti wa Kitongoji hicho kwa madai ya Uchochezi.Pia amewataka Wananchi wa Kitongoji hicho kuendelea na Majukumu yao Kama kawaida
Comments