WATOTO WASIMULIA JINSI MJOMBA WAO ALIVYOWALAWITI


 Jeshi la Polisi mkoani hapa linamsaka mkazi wa Nyarugusu, Masumbuko Sumbu (16) kwa tuhuma za kuwalawiti ndugu zake watatu wenye umri wa miaka 10 na mwingine minane.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Geita, Henry Mwaibambe amekiri kuwa Sumbu ambaye anajihusisha na shughuli za uchimbaji madini anatuhumiwa kuwalawiti watoto hao ambao ni wajomba zake anaoishi nao nyumbani kwa babu yao Kata ya Bukoli.

Wakizungumza na Mwananchi Digital watoto hao(majina tumeyahifadhi) wamedai kuwa, binamu yao huyo amekuwa akiwaingilia kinyume na maumbile kwa muda mrefu, lakini waliogopa kusema kutokana na kuwatisha kuwa atawaua.

“Usiku ukiingia kila mtu akiwa amelala anatuamsha na kutuambia tuvue nguo kisha anashusha suruali… anatuinamisha kwa zamu akitoka kwangu anakwenda kwa mwingine hadi wote watatu anapomaliza ndio analala,“ amesema mmoja wa watoto hao.

Amesema binamu yake anayeishi maeneo ya Nyarugusu alianza kumlawiti akiwa darasa la pili na ndugu yake mwingine; na sasa ameanza kumuingilia mdogo wao wa miaka minane.

Watoto hao wanaoishi na babu na bibi yao wameiomba Serikali kumchukulia hatua binamu yao kwa kuwa hawajui akirudi atawafanya nini kwa sababu alishaahidi kuwaua endapo watatoa siri

Pia Mwalimu wa darasa la tatu, Moses Luheja amesema siku ya tukio majira ya saa nne wakati wakiwa mapumziko mmoja wa watoto hao alienda kujisaidia, lakini eneo la haja kubwa lilitoka kitu kama utumbo mpana ukiwa umejaa kama puto na kushindwa kusimama akalazimika kukaa chooni kwa muda wa nusu saa.

“Tulimkuta amechoka kuchuchumaa chooni muda mrefu tukakuta kitu kinaning’inia mithili ya puto nikarudi ofisini kumchukua mwalimu mwingine na khanga ya mwalimu wa kike tukambeba kwa kuwa alikua hawezi kuvaa suruali tukaita pikipiki na kumpeleka kituo cha afya akapewa huduma ya kwanza.

Mganga Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Afya Bukoli, William Dati amekiri kumpokea mtoto huyo akiwa ametoka kitu sehemu ya hajakubwa huku wengine wawili wakiwa na michubuko na damu sehemu za haja kubwa.


Solanya Mhozya ambaye ni babu anayeishi na watoto hao amesema hakujua vitendo hivyo vinafanyika nyumbani kwake kutokana na wajukuu kuhofia kutoa siri.

Diwani wa  Bukoli, Faraji Seif amesema kata yake ina matukio mengi ya ukatili na kuomba taasisi zinazojihusisha na ukatili wa kijinsia kutoa mafunzo kwa wakazi wa eneo hilo.

Pia, amewataka wazazi kuona umuhimu wa kuishi na watoto wao badala ya kuwaachia babu na bibi na kuwataka kujenga utamaduni wa kuwafuatilia na kujua afya zao

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE