RAIS SAMIA AONYA UKABILA NA UDINI
Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuna kazi ya kuirudisha nchi kuwa moja baada ya kutetereka kwa watu kujuana kwa udini, kabila, ukanda na itikadi.
Rais Samia ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 9, 2022, kwenye mdahalo wa kitaifa kuadhimisha miaka 100 ya kuzaliwa kwa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, uliofanyika katika shule ya Uongozi Kibaha Mkoani Pwani.
Aidha amesema Mwalimu Nyerere amewaachia somo kubwa Watanzania la kuwa wazalendo na Taifa kwani alilipenda taifa lake, na kujitoa mhanga kwa ajili ya watanzania.
“Uzalendo wa Mwalimu Nyerere ulijidhihirisha tangu nyakati za kupigania uhuru, ambapo aliamua kuacha kazi yake ya ualimu ili ajikite zaidi kwenye kazi za kupigania uhuru na atukomboe Watanzania wenzie na akapitia magumu na changamoto nyingi kwa ajili ya kulikomboa taifa hili,” amesema Rais Samia.
Kuhusu lugha ya Kiswahili, alisema Mwalimu Nyerere aliiwezesha kukubalika wa Waafrika na sasa ni lugha rasmi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Utamaduni (Unesco) kuitengea siku yake maalumu
Comments