UJENZI STENDI YA MKOA SONGWE YAOTA MBAWA,ENEO LAVAMIWA NA KILIMO

 

WANANCHI "TUNAWAOMBA TAKUKURU SONGWE IFUATILIE ENEO LA STENDI YA MKOA NANI KARUHUSU WATU WALIME WAKATI PALISINDILIWA VIZURI KWA KODI ZETU BORA WANGEWEKA HATA MRADI WA MUDA PALE"

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Songwe imeombwa na wananchi wa Wilaya ya Mbozi kufuatilia eneo lililoombwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Songwe mbele ya Rais DKT JOHN P. MAGUFULI ijenge Stendi ya Stendi ya Mkoa kisha na kubadilishiwa matumizi ya eneo hilo na Rais.
Ikumbwe wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana 2020 Chama cha Mapinduzi kilitumia eneo hilo kwa Mgombea wake wa Urais kuomba kura kwa Wana Songwe na hii ilitokana na uwingi wa watu waliokuwa wanajitokeza katika mikutano yake nchi nzima.
Wakati wanasongwe wakiwa na shauku ya kuanza ujenzi wa eneo hilo Mara moja na tayari eneo hilo lilikuwa kiasi flani limetengenezwa kwa kusafishwa na kumwangwa kifusi lakini hali imekua tofauti na matarajio ya wengi eneo hilo hivi sasa limevamiwa kwa kilimo na wananchi.
Wananchi wapenda maendeleo wamemtafuta Mwandishi wetu na kutoa malalamiko yao huku wakidai hawapendi kuona Kodi zao zikichezewa kiasi kila na wakaenda mbali sana kuwa Mkoa wa Songwe hauna uhaba wa maeneo ya kulima kiasi kwamba leo watu wakalime eneo lililotengwa kwa matumizi ya maendeleo ya Mkoa.
"Hivi kweli leo hii waseme sasa tunaanza kujenga stendi ya Mkoa kwa hiyo waanze kukata mazao ya watu? hizi ni tamaa za watu wachache wamekodisha lile eneo kwa watu walime je hizo fedha zipo wapi? Hapana hapa Takukuru waingilie kati huku ni kuchezea fedha za umma'-John Kitabuje
Mwananchi mwingine ambae ni mtumishi maeneo hayo aliomba jina lake lihifadhiwe alidai njia hiyo wanapita Viongozi kila siku je hawayaoni hayo yanayojili eneo hilo.
"Tumepewa zawadi ya eneo lakini cheki leo tunavyoaanza kufanya hivi alietupa eneo kesho akipita hata na kukuta haya si ataona kuwa hatuna shida na eneo hilo sie"Pamoja na yote wananchi walimtaja aliekuwa Meneja wa kuwa ndie aligawa hayo maeneo kwa ujira flani na tulimtafuta Meneja huyo na kumuuliza kuhusu yeye kugawa maeneo hayo na tulimpata kwa njia simu.Meneje huyo anefahamika kwa jina la Lyson Mbwaga alidai kila kitu aliekuwa Mkurugenzi na halmashauri ya Mbozi Godigodi hivyo hana majibu

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE