UNYWAJI POMBE NA BANGI WAKATI WA UCHIMBAJI MAKABURI MBOZI WALALAMIKIWA
Wakazi wa Wilaya ya Mbozi wamelalamikia tabia ya Vijana ilioibuka Miaka ya hivi Karibuni ya Uvutaji bangi na unywaji pombe kali ilioibuka katika Mazishi mbalimbali Wilayani Mbozi.
Wakiongea na Kituo hiki cha habari Wakazi wa Mbozi hususani kata za Vwawa,Ilolo,Isangu na Ichenjezya wamedai kuwepo kwa baadhi ya matukio ya kufafana ya Uuzaji wa pombe kali na Uvutaji wa bangi pindi Misiba inapotekea hususani maeneo ya Makaburini ambapo shughuli za uchimbaji wa makaburi unapofanyika.
Aidha Wakazi hao wamedai kumekuwa na tabia ya baadhi ya Vijana wanaposikia mahali kuna msiba hususani kata hizi basi wapo Vijana hujumua pombe kali( hususani zilizopigwa marufuku) na wauza bangi huwahi eneo la kuchimbia Kaburi huko hukutana na Vijana watumiaji wa Vilevi hivyo na hutumia Kwa uhuru zaidi kama wanavyodai wenyewe kwani hakuna usumbufu waupatao kutoka kwa mamlaka husika zinazosimamia Sheria.
"Kwa kweli tabia hii ya Uvutaji bangi na Ulevi wa kupindukia kwa Vijana wetu huko Makaburini imeshamili sana wanajisahau kabisa kama Mazishi ni Ibada matokeo yake yanapofanyika Mazishi wao huwa watu wa kupiga kelele na kuwakosea adabu Viongozi wetu wa kiroho" amelalamika Mkazi wa Ichenjezya na ambae aliomba jina lake lihifadhiwe
Aidha wamewaomba Vijana wao kwa wao kuwa utaratibu maalumu ya kuheshimu Mazishi na taratibu za Ibada na kuhakikisha hawawakosei adabu wafiwa.
Aloyce John Mkazi wa Mbeya ambae yupo Mbozi katika Msiba wa Ndugu yake ameshangazwa na kitendo cha Vyombo vya Dola kuwaacha huru Vijana hao wanaonekana kuharibikiwa afya zao na Uvutaji wa bangi na pombe kali eneo la wazi Makaburini na kuonekana ni kero kwa waombolezaji na wafiwa na ameomba Vyombo vya Dola kuchukua hatua.
Kwa upande wa Joseph Mwamtego( sio jina lake halisi) amedai kuwa yeye biashara yake kubwa ni pombe kali kama Win na zingine toka Malawi pindi asikiapo Msiba huwahi Makaburi na huakikisha amejumua Vinywaji vya kutoka kwa wateja wake ambao huwakuta huko.
Mchungaji wa Kanisa moja lililopo katikati ya Mji wa Vwawa ameiomba Serikali kupitia Vyombo vyake kuhakikisha wanaikomesha tabia hiyo ilioibuka kwani Kwa Upande wao inawakera sana na ni kumkosea Mungu na Marehemu adabu
Comments