WANAUME WA RUKWA WAMEHARIBIKA VIUNO-MBUNGE


 Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bupe Mwangata amesema matuta yaliyopo katika barabara za Rukwa yamekuwa yakiharibu viuno vya wanaume wa mkoa huo.

Bupe amesema barabara ya kutoka Tunduma hadi Sumbawanga Mjini ina matuta mengi ambayo yamesababisha viuno vya wanaume wa mkoa wa Rukwa kutofanya kazi vizuri.

“Serikali inapata ugumu gani wa kuondoa yale matuta? Yale matuta yanatuletea matatizo yale matatizo ni makubwa sana, hata kwenye magari yanaharibika,”amesema.

Amesema barabara hiyo imekuwa ni tegemeo kwa uchumi wa Taifa.

Hata hivyo mmoja wa wabunge alisikika (ambaye hakutajwa) akimpatia taarifa Bupe kuwa ni kweli kwamba barabara hiyo imesababisha wanaume wa Mpanda waliomo ndani ya Bunge walalamikie viuno.

“Nataka kumpa taarifa kuwa ni kweli hoja ya matuta na viuno kwa wanaume wa Mpanda wamethibitishwa wanalalamika sana humu ndani ya hili jengo (bungeni),”amesema mbunge huyo na kusababisha vicheko kwa wabunge.

Akiendelea kuchangia Bupe, alisema kuwa anapokea taarifa hiyo kwa mikono miwili kwasababu amewaona wanaume wa mkoa wa Rukwa wanavyopata shida na matuta hayo.

Amesema kuwa nyumba nyingi zinavunjika na chanzo ni matuta hayo yaliyowekwa barabarani.

Amesema Rais John Magufuli wakati wa uhai wake alimuagiza waziri anayehusika na ujenzi kuondoa matuta hayo ndani ya mwezi mmoja lakini agizo hilo halikutekelezwa.

Amesema hata Katibu Mkuu wa CCM (hakumtaja) alipofanya ziara mkoani humo hakulala usiku mzima kwa sababu ya shida ya mgongo aliyoipata kutokana na matuta hayo.

Amesema Katibu huyo alitoa maagizo ya kuondolewa kwa matuta hayo ndani ya wiki mbili agizo ambalo pia halikutekelezwa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE