ZAHANATI ILIOJENGWA KWA MAMILIONI MBOZI YADAIWA KUTELEKEZWA,


 Wananchi wa Kijiji cha Isowenzya kilichopo kata ya Isansa wamedai kukosa huduma za kiafya baada ya Zahanati  iliyopo Kijijini hapo kutotowa huduma Kwa muda mrefu hali iliopelekea Zahanati hiyo kufungwa muda mrefu.


Wananchi hao wameishukuru Serikali Kwa kuwajengea Zahanati hiyo yenye hadhi kubwa lakini huduma kwao zimekuwa hazipatikani hivyo wanaiomba Serikali kuwasaidia kwani wanapata tabu kutokana na kukosekana huduma ya matibabu kituoni hapo.

Moja ya Majirani waliokizunguka kituo hicho wamedai kuna mtoa huduma mmoja tu na Serikali imemjengea mpaka nyumba lakini vyote vimetelekezwa na hawaoni dalili ya wao kupatiwa wataalamu wa afya.


"Kama mnavyoona Zahanati hii imetelekezwa mtoa huduma inaweza hata kufika miezi mitatu hajafika kutoa huduma na hatujui anaishi wapi wakati nyumba ya mamilioni kajengewa hapa lakini hayupo"alilalamika Mwananchi wa Isowenzya alifahamika kwa jina moja Mama Ima

Aidha kituo hiki cha habari kimemtafuta Mganga wa Wilaya Mbozi Mponjoli Mwangosi ambapo amedai ni kweli tatizo la Zahanati hiyo analo na amemjulisha mpaka Mheshimiwa Diwani  Sikudhani Mbwaga wa kata hiyo na kubwa ni mtoa huduma wa kituo hivyo ni  dhaifu kiafya na kutokana na Serikali kutangaza ajira za Afya wanategemea pindi mchakato utakapokamilika watahakikisha wanawapeleka wataalamu kituo hapo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE