RC SONGWE AWATAKA WAKUU WA WILAYA KUJIRIDHISHA KABLA YA KUWAWEKA WATU NDANI
Mkuu wa Mkoa ametoa wito huo kwenye maadhimisho ya sikukuku ya wafanyakazi ambayo kwa ngazi ya Mkoa imefanyika katika Mji wa Tunduma, 1 Mei 2022.
"Lazima tujiridhishe kosa linaloweza kuhatarisha Amani ya sehemu hiyo au usalama wa Taifa na ukimweka ndani kwa adhabu hiyo hakikisha anatakiwa apelekwe Mahakamani" Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba.
Mkuu wa Mkoa amesema kama kuna mtumishi amefanya kosa la jinai lazima akamatwe na apelekwe Mahakamani lakini kama ni kosa la kiutumishi ni lazima lirudi katika mamlaka yake ya utumishi ili wamchukulie hatua za kinidhamu
Aidhaa, Mkuu wa Mkoa amesema wakati mwingine mtu anawekwa ndani kwa sababu ya usalama wake baada ya Serikali kujiridhisha usalama wake uko hatarini.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa ametoa vyeti kwa Wafanyaki bora katika kada mbalimbali.
Maadhimisho hayo yalihudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Mkoa na Wilaya.
Comments