BREAKING NEWS: GARI LA OFISI YA RC SONGWE LAKAMATWA KWA MAGENDO
Magari 14 yamekamatwa katika Oparesheni Maalumu ya kupambana na magendo katika Mpaka wa Tunduma kupitia Kamati ya ulinzi na Usalama iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe.
Kati ya Magari hayo 14 ambayo yamekamatwa gari moja linamilikiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe likiwemo gari ambalo limekuwa likitafutwa kwa miaka mingi bila Mafanikio.
Hapa Rc Mgumba anatoa msimamo wa Serikali juu ya magari yaliyokamatwa na wale wote watakao kamatwa na magendo kwa mkoa wa Songwe.
Aidha Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe ametoa wito kwa Wafanyabiashara, kufuata sheria za forodha na kueleza changamoto wanazopata wakati wa kudhibiti magendo katika Mpaka wa Tunduma.
Comments