GARI LILILOBEBA MAGENDO LAPATA AJALI SONGWE LIKIWAKIMBIA KIKOSI KAZI CHA MKOA WA SONGWE

Gari aina ya Brevis lenye namba za usajili T 265 CYN limepata ajali maeneo ya Ichenjezya Vwawa Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe likiwa limebeba Magendo mbalimbali vikiwemo Vipodozi na Vitenge.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Jumapili ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wamedai gari hilo lilikuwa mwendo kasi na limezima taa na ndipo lilipokuta na tuta lililopoka katika barabara hiyo na kisha kupaa na kudondoka huku matairi yakielekea juu.

Akitoa taarifa Meneja wa Tra Mkoa wa Songwe Dikson Qamala amesema gari hilo lilikuwa nikiwakimbia kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na Magendo kilichoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Mgumba.

"Hili gari lilikimbia kizuizi chetu tulichokiweka Oldvwawa na kukigonga ndipo lilipopasua matairi yake mawili na katika kututoroka alikimbilia njia ya Ichenjezya na ndiko alipopata hii ajali na pia kuna gari  tumelikamata aina ya Crown T 510 DYC ambalo lilikuwa likiisindikiza gari iliopata ajali na lenyewe tumelikamata na Vitenge na Vipodozi" amesema Dikson Qamara Meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Songwe TRA.

Hata hivyo wamesema hawakuweza kufanikiwa kuwakamata Madereva wa Magari yote mawili baada ya kutoroka. aidha Qamara ametoa wito kwa Wananchi wote wanaojihusiha na Vitendo vya kusafirisha au kuuza na hata kununua kuacha tabia hiyo mara moja na kufuatia taratibu za ulipaji kodi na wao Tra wapo tayari kuwahudumia na kuwapatia Elimu kwani kwenda kinyume na taratibu ni kuikosesha Serikali mapato.

Hivi Karibuni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe Omary Mgumba aliunda kikosi maalumu ndani ya Mkoa wa Songwe kitakachoshughulikia kuzuia na kupambana na Magendo Ili kuweza kukomesha biashara ya Magendo Mkoa wa Songwe

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE