POLISI SONGWE WATOA SABABU ZA MFANYABISHARA SONGWE BARAKA SANGA KUJINYONGA



 Jeshi la Polisi Mkoani Songwe limetoa taarifa ya kifo cha kujinyonga cha Kijana Maarufu Mkoani Songwe na Mfanyabiashara anaefahamika kwa jina la Baraka Sanga maarufu kwa jina la  Twangara aliejinyonga kwa kutumia Shuka jeupe.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Jannet Magomi amesema Baraka  Sanga amekutwa amejinyonga mida ya saa kumi na mbili na robo asubuhi kwa kutumia Shuka.

"Tumepata taarifa ya Kujinyonga kwa Kijana anaeitwa Baraka Isack Sanga Kabila lake Mkinga katika kata ya Ilolo amejinyonga na taarifa zetu za kiuchunguzi marehemu amejinyonga kutokana na Ulevi wa kupindukia baada ya kuachwa na Mkewe na Marehemu hakuacha Ujumbe wowote" amesema kamanda wa Polisi Songwe Jannet Magomi.

Baraka Sanga alikuwa ni Mfanyabiashara wa Duka maeneo ya njia panda ya Kuelekea Stendi ya Starehe Wilayani Mbozi na alikuwa maarufu kutokana na Ucheshi wake mbele ya Jamii hususani Vijana.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Pumzika Kwa Amani Baraka Sanga





Comments

Popular posts from this blog

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

CONSTRUCTION OF THE ISONGOLE-ISOKO ASPHALT ROAD IS NOW OFFICIAL, CONTRACTOR INTRODUCED TO THE PUBLIC

MBUNGE MOMBA KUTOA SHILINGI MILIONI 28 UJENZI WA OFISI ZA CCM KATA 14