DED ILEJE ANAEDAIWA KUJIUZIA GARI LA SERIKALI KWA MILIONI 4 AIBUKA NA MAZITO


Kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba kumuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Missaile Musa kumuita aliekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje Haji Mnasi kwa madai ya kujiuzia gari la Serikali aina ya Toyota Hilux yenye namba za usajili DFPA 8508 kwa thamani ya milioni 4 tu gari lilotembea kilometa 900 Mkurugenzi huyo ameibuka na kutoa ufafanuzi.

Akiongea Kwa njia ya Simu Mnasi ameshangazwa na madai hayo na amekiri kuyasikia 

"Ni kweli nimepata simu za wadau mbalimbali zinazohusiana na tuhuma hizo kiukweli mimi sijanunua hilo gari na lipo Ileje kwenye yadi ya Wilaya na Mimi ndie niliyezuia gari hilo kununuliwa na mnunuzi mmoja aliekuja na kibari toka Wizarani na nikalieleza baraza la Madiwani uwamuzi wangu wa kulizuia gari hilo kuuzwa' amesema Mnasi


Aidha Mnasi amedai kuwa mpaka yeye anaondoka Ileje gari hilo kaliacha Ileje na madai dhidi yake ni upotoshaji na hata miutasali ya Vikao vya Baraza la Madiwani vina maelezo ya alichokisema ndani ya Baraza juu ya gari hilo alilolizuia kuuzwa kwa kibari toka Wizarani kilichompa mnunuzi   mamlaka ya kununua gari hilo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE