DED SONGWE YAMKUTA MAZITO MBELE YA RC SONGWE


 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ametoa masaa 12 kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Songwe kutoa maelezo kwa maandishi ya kuchelewesha mradi wa kituo cha Afya Ifwenkenya,


Mgumba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi


Aidha mgumba amewakumbusha Viongozi Wilayani humo kuzingatia  maelekezo   ya Mh Rais kwa Kiongozi ambaye hatawajibika katika utekelezji wa miradi ya maendeleo kwamba kwanini asichukuliwe hatua kwa kutokamilisha hatua za ukamilishaji wa vituo vya Afya 




Aidha katika Hatua nyingine Mgumba amewaaagiza Viongozi Wilayani humo kuhakikisha wanajenga mradi huo usiku na mchana  ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati pamoja na kuwasilisha taarifa ikiwa na miongozo ya ujenzi wa miradi na manunuzi ya vifaa vya ujenzi (BOQ)


Ziara ya Mkuu wa mkoa huo ni muendelezo wa Ziara zake za kikazo Mkoani humo zilizolenga kukagua miradi ya maendeleo na kusikilia kero za Wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE