HALMASHAURI YA MOMBA YAMKUNA RC YAOKOA MAMILIONI YA FEDHA MBICHI...RAS AKABIDHIWA RUNGU LA WADAIWA


Halmashauri ya Wilaya ya Momba katika kipindi cha Miaka 7 imekuwa inakabiliwa na changamoto ya Kutopeleka fedha za makusanyo ya  Mapato Benki hadi kufikia kiasi Cha  zaidi ya shillingi Milioni 800 kuanzia Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 hali iliyopelekea Wilaya kuwa na hoja ya kujirudia kila Mwaka.

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Regina Bieda ameyasema hayo katika Baraza la kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Juni 25, kuwa tangu  2021 awe katika nafasi hiyo alibaini tatizo hilo na kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika kwenye kukusanya fedha za Mapato bila kuweka Benki na hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuajiri vibarua wapya na kupewa mashine za POS ambazo zilikuwa zinatumiwa na watendaji wenye madeni ya Fedha mbichi ili kupisha Watendaji hao kuwa huru na Kuendelea na kesi zao bila kuathiti mapato ya Halmashauri.

"Kuanzia 2021 Halmashauri tumefanikiwa kudhibiti mapato yanayokusanywa bila kuweka Benki, hadi Juni 2022 hatuna tena fedha mbichi kama Halmashauri ila bado tunazidi kukusanya fedha  kwa wadaiwa kutoka milioni 800 za awali na kufikia milioni 501 za sasa haya yote ni madeni ya kuanzia 2016/2017 hadi 2019/2020" Bi. Regina Bieda.


Aidha Bieda amesema wadaiwa 28 ambao madeni yao ni Milioni 242,724,312  tayari wamefikishwa Mahakamani ambapo  wadaiwa 3 ambao madeni yao ni Milioni 83,347,543 wamefunguliwa mashauri ya jinai katika mahakama ya Wilaya hiyo na wadaiwa 21 ambao madeni yao ni Milioni 657,084,838 wamefunguliwa makosa ya madai katika Mahakama ya Mwanzo Tunduma.


Pia, wadaiwa 2 ambao madeni yao ni milioni 44,518,980  wamekubaliana na madeni na wamepewa muda ili waweze kurejesha fedha hizo.


Aidha, wadaiwa 25 waliobaki wanadaiwa milioni 285, 157,067.00 wameandikiwa Barua ya kusudii la kuwashitaki inayo wataka warejeshe fedha hizo na wakishindwa tutawapeleka Mahakamani kwa makosa ya madai kwani walivunja makubaliano ya ulipaji wa fedha hizo.


Kufuatia hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Omary Mgumba ametoa siku 7 kwa watu wote ambao wanadaiwa fedha izo wawe wamelipa kwenye Halmashauri.


Aidha, Mkuu wa Mkoa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa, Ndg. Missaile Musa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mtalamu wa mapato na ajieleze kwa nini asiondolewe kwenye nafasi yake kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo hazijawekwa Benki wakati yeye anaweza kuona muda wowote fedha iliyoingia.


Kitendo cha Halmashauri kuwa na fedha nyingi kutowekwa Benki kunachelewesha maendeleo kwa wananchi hivyo lazima hatua zichukuliwe kwa wote wanaodaiwa.


#JIANDAE KUHESABIWA

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE