ASKARI ALIYEMTESA MTUHUMIWA AKIWA KUFUNGWA PINGU AKAMATWA

 Jeshi la Polisi nchini Tanzania limeonya vitendo vya baadhi ya askari wake kuwapiga watuhumiwa na kusisitiza hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.



 Hili limekuja kufuatia kusambaa kwa video mitandaoni inayomuonyesha askari akimpiga mtuhumiwa aliyeiba simu na kukiri kufanya tukio hilo na kuonyesha mtu aliyemuuzia simu hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Agosti 23, 2022 na Msemaji wa jeshi hilo, David Misime imeeleza askari huyo tayari ameshachukuliwa hatua na sasa yupo mahabusu.

Misime amesema kitendo hicho si tu kinyume cha sheria bali ni kinyume na maadili ya Jeshi la Polisi hivyo hatua za kinidhamu dhidi ya askari huyo zitachukuliwa

“Tukio hilo limeshachukua hatua kuanzia jana na kamanda wa Polisi Kinondoni, askari aliyehusika yupo mahabusu na hatua stahiki zinaendelea kuchukuliwa dhidi yake,” amesema na kuongeza:

“Jeshi la polisi litaendelea kusimamia nidhamu, haki, weledi na uadilifu kwa kuchukua hatua stahiki dhidi ya askari anayekiuka sheria na maadili,” amesema Misime.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA