DED MUHEZA ASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga (DED), Nassib Bakari Mmbaga kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa na Tamisemi leo Jumanne Agosti 30, 2022 imesema Waziri Bashungwa amechukua hatua hiyo baada ya mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo sambamba na utendaji kazi usioridhisha.

Taarifa hiyo imesema Mmbaga amesimamishwa kazi kuanzia Jumanne ya Agosti 30, 2022

Waziri Bashungwa amewataka wakurugenzi wa halmashuri zote nchini kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo kikamilifu.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE