MABILIONI YAPELEKWA JESHI LA POLISI KUNUNUA MAGARI YA MAKAMANDA
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amesema, Serikali imetoa Sh15 bilioni kwa ajili ya kununua magari yatakayopelekwa kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa (Ma-RPC).
Aidha, magari hayo yatakwenda kwa makanda wa polisi wa wilaya (Ma-OCD) na fedha ya mafuta itakayokwenda moja kwa moja wilayani ili kurahisisha utendaji kazi za Polisi.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Agosti 25, 2022 na Waziri Masauni wakati anafunga mafunzo awali ya polisi kozi namba moja ya 2021/2022 katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi Mkoa wa Kilimanjaro.
Waziri huyo amewataka askari wahitimu kuwaheshimu Watanzania ikiwa ni pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa wakati na kwa haraka.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Polisi Tanzania, Ramadhani Mungi amesema shule ilipokea zaidi ya wanafunzi 4,310 na waliohitimu mafunzo hayo ni 4,122 huku wengine 186 wakiachishwa mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.
Aidha, wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya nadharia na vitendo.

Maoni